Timu mbalimbali duniani kwa sasa zipo katika harakati za usajili huku nyingine zikiandaa programu za mazoezi kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.
Mbali ya maandalizi hayo, baadhi ya timu husasan za England na Hispania zipo katika hatua za mwisho kuandaa mechi za maandalizi kwa lengo la kuwaweka sawa wachezaji wao ambao kwa sasa wapo mapumzikoni.
Ni jambo la kawaida kwa timu ya Arsenal, Manchester City, Liverpool, Tottenham, Chelsea na Manchester United kufanya ziara mbalimbali nje ya nchi yao na mara nyingi sana upendelea kutembelea nchi za Mashariki ya mbali. Also Read
Wakati timu hizo zipo katika mikakati hiyo, mashirikisho ya soka nayo yanatumia muda huu wa mapumziko kufanyia marekebisho baadhi ya sheria ikiwa lengo kubwa ni kuziboresha.
Hatua ya kuziboresha sheria za soka imeanzia Fifa na chombo cha kutunga sheria hizo, IFAB na mpaka sasa sheria mbalimbali zimefanyiwa marekebisho kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.
Kwa mujibu wa IFAB, sheria namba 12 ambao ni maalum kwa makosa na utovu wa nidhamu (Fouls and Misconduct) nayo imefanyiwa marekebisho.
Sheria hii imefafanuliwa zaidi na kupunguza makali kwa kocha au meneja timu ambaye atakiuka matumizi ya eneo la ufundi. Kwa marebisho ya sasa kocha au meneja hawezi kuadhibiwa kwa kosa lililofanywa na mchezaji na kukiuka aneo lake.
Mbali ya uboreshwaji huo, pia sheria namba 14 inayohusiana na pigo kubwa maarufu kwa jina la penalty nayo imeongezewa ‘nyama’ na kuwabana zaidi makipa ambao mara nyingi uwapa vitisho wapigaji penalty kwa lengo la kuwachanganya au kuwapanikisha.
Ufafanuzi wa sheria hii ni kwamba kipa hapaswi kuwa na tabia ya kumtisha mchezaji aliyechaguliwa kupiga penalty kwa matendo yenye lengo la kumvuruga’ mpigaji.
Pia upande wa Mwamuzi Msaidizi wa Video (VAR) nao umeguswa ambapo mfumo wa ‘VAR ‘Light’ hauhusishi kurudiwa kwa tukio yaani replay.
IFAB pia imefanyia maboresho sheria namba tatu inayohusiana na wachezaji (Players). Sehemu ya tisa ya sheria hiyo imetoa ufafanuzi na kuboreshwa kuhusiana na goli au bao lililofungwa huku ndani ya uwanja kukiwa na mtu ambaye hausiki na mechi husika kwa mujibu wa sheria.
Mtu huyo anaweza kuwa shabiki au viumbe wowote ambapo kifungu hicho kimepa mamlaka mwamuzi kuamua nini cha kufanya kutokana na mazingira yaliyokuwepo.
Mfano, mara baada ya bao kufungwa na mwamuzi kugundua kuwa kulikuwa ma mtu wa ziada ndani ya uwanja anatakiwa kuamua ifuatavyo”-
Kukataa bao lilolofungwa endapo mtu wa ziada alikuwa ameingilia mchezo kwani sheria ina mzuia kuingia uwanjani tofauti na wachezaji 22 walioruhusiwa.
Endapo mtu wa ziada alikuwa ni mchezaji wa akiba, mchezaji aliye adhibiwa kwa kadi nyekundu, aliyebadilishwa (substituted player) au kiongozi wa timu ambayo imefunga bao, jukumu la mwamuzi ni kukataa bao hilo na kuanza mchezo kwa pigo la moja kwa moja (direct Freekick) kuanzia eneo ambapo mtu wa ziada alikuwepo.
Pia, Endapo mtu wa ziada hausiani na timu yoyote, mwamuzi atatakiwa kuanza mpira kwa dropped ball.
Vile vile, Mwamuzi anaweza kukubali goli kuwa halali endapo mchezaji, mchezaji wa akiba, mchezaji wa akiba aliyetoka nje ya eneo la kuchezea, mchezaji au kiongozi aliye adhibiwa kwa kutolewa nje anahusiana na timu ambayo imefungwa bao.
Marekebisho au uboreshwaji wa sheria mbalimbali zipo nyingini, ila kwa leo tuishie hapa…
Chukua hii
Wakati Bodi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara (TPLB) na Shirikisho la Soka nchini (TFF) wanaandaa kanuni mpya za Ligi za msimu ujao, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Mrisho Kikwete ameonyeshwa kukerwa na wachezaji wa kigeni kutawala soka la Tanzania.
Kikwete pia ameishauri Serikali kukaa na TFF kuweka mkakati wa kuzalisha wachezaji bora wazawa mbao watakuwa nyota katika ligi yetu na kusaidia timu ya taifa pia. Kazi inabaki kwa TFF na TPLB katika mchakato wa kanuni za msimu ujao wa ligi.