Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hivi ni kweli tunaheshimu mpira wa miguu?

YANGA BIGIRIMANA MORRISON MAYELE Hivi ni kweli tunaheshimu mpira wa miguu?

Mon, 17 Oct 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Nimeshtuka sana wiki hii kumsikia Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohammed Mchengerwa, akitoa maagizo Yanga ikashinde Sudan! Nimeshituka sana.

Soka ni mchezo usiondeshwa kwa maagizo. Timu za soka zinafanya kazi kwenye mazingira tofauti sana.

Sio kweli Yanga ilitaka kupata sare nyumbani. Sio kweli. Ilifanya kila inachoweza lakini uwezo wao uliishia kwenye sare.

Lakini ifike mahali tuwe na heshima kwa soka. Tatizo kubwa kwa viongozi wetu wakati mwingine wanapenda kuongee sana.

Tatizo kubwa la viongozi wetu wanataka kuongea kila wanapoona watu wako mbele yao. Serikali ina mambo yake ya msingi inayopaswa kuyatekeleza kabla ya kujiingiza kwenye klabu za Simba na Yanga.

Yawezekana nia ilikuwa ni njema kabisa ya Waziri Mchengerwa lakini soka haliendeshwi kwa maagizo kama aliyoyatoa.

Hakuna mtu nchini anayetaka Yanga itolewe, lakini matokeo ya awali ndio yanawapa watu kigugumizi. Hakuna anayetaka kuona wawakilishi wetu wa nchi kimataifa inaondoka mapema. Hakuna.

Hata Simba yenyewe ingependa Yanga apite ili waendelee kutambiana kila Wikiendi. Waziri apunguze kidogo amri. Labda nia yake ilikuwa njema, lakini maagizo na maelekezo hayajawahi kusaidia kwenye soka.

Ukimsikiliza waziri, kuna muda unapata kigugumizi. Ukimsikiliza waziri, kuna muda unapata sentensi tata. Labda nia yake ilikuwa njema, lakini kuna maneno sidhani kama ni sawa kuzungumzwa na kiongozi mbele za watu.

Ukisema TFF wasitoe mbinu za kushinda kimataifa kwa timu moja tu waisaidie na Yanga, ni utata wa hali ya juu.

Nia yawezekana ni njema, lakini kauli kama hizi hazijakaa vizuri.

Tatizo la soka la Bongo bado limejikita sana kwenye mchanganyiko wa siasa za Simba na Yanga.

Tatizo la mpira wetu kwa kiasi kikubwa sana bado siasa za nchi zimejikita ndani yake.

Simba na Yanga ndio wahamasishaji wakubwa wa Sensa. Simba na Yanga ndiyo wahasishaji wakubwa wa wapigakura! Hapa napo bado tunafeli sana.

Serikali ingeacha kuingilia mambo ambayo kimsingi sio jukumu lao. Serikali haina jukumu la moja kwa moja kwenye klabu. Wao wangejikita tu kwenye timu za Taifa.

Unapokuwa na taifa linalotoa timu nne kwenye ushiriki wa kimataifa halafu ukaja kutoa maelekezo kwa timu moja tu, watu watakushangaa! Kwa nini ni Yanga tu na sio timu nyingine? Hakuna majibu.

Kama kweli serikali inataka kusaidia klabu zetu, ni jambo jema. Waje sasa watoe msaada, sio maneno matupu!

Hadi sasa ulitakiwa usikie serikali imetoa ndege kusafirisha Yanga kwenda Sudan. Hadi sasa ulitakiwa isikie serikali imelipia kambi ya Simba inayojiandaa na mechi ya Primeiro de Agosto.

Serikali ingeviacha klabu viendelee kujiendesha kuliko kuja kupiga siasa kila siku.

Yanga haiwezi kufuzu kwa sababu ya maneno ya waziri. Hata siku moja haiwezi kutokea. Soka ni mchezo wa maandalizi na uwezo. Yanga itafuzu kwa sababu za uwezo wao uwanjani, sio maelekezo ya waziri. Siasa na mpira ni mambo mawili tofauti. Serikali ingejikita kwenye kutengeneza sera nzuri za michezo, kuboresha miundombinu ya michezo, kuandaa watalaamu nk.

Haya ndiyo yanapaswa kupewa kipaumbele na serikali. Huku ndiko serikali inapaswa kuweka nguvu. Mambo ya Simba na Yanga wangeachana nayo kabisa. Waziri anatengeneza maswali mengi kuliko majibu kwenye kauli zake. Sidhani kama imekaa vizuri.

Soka hauataki maagizo. Soka na michezo kwa jumla ni maandalizi na uwezo. Nimeshangaa sana kumsikia waziri akitoa maagizo utadhani Yanga inaenda kujenga barabara ya kwenda Kilwa.

Nimeshangaa sana kuona serikali inataka kujiingiza kwenye mambo ambayo kimsingi hawahusiki moja kwa moja.

Tatizo la mwanasiasa, kila jukwaa mbele yake anataka liwe fursa. Kila anapoona watu wengi mbele yake, anatamani kuwahutubia!

Soka letu haliwezi kuendelea kwa kupewa maagizo ya serikali. Hadi sasa ukizitafakari kauli za waziri, unaona kuna maswali mengi kuliko majibu!

Serikali inaeneo kubwa sana la kusaidia soka letu kabla ya kuja kupiga hizi porojo kwenye klabu zetu za Simba na Yanga. Tangu nchi hii imepata Uhuru, michezo haijawahi kuwa kipaumbele cha taifa kwenye bajeti.

Tangu tumepata Uhuru, michezo haijawahi kuwa namba moja kwenye nchi lakini kuna mafanikio tunayo.

Watu kama kina Suleiman Nyambui, Filbert Bayi, Alphonce Simbu, Habib Kinyogoli, Mbwana Samatta na wengine wengi wameliheshimisha sana taifa letu. Nadhani umefika wakati kama taifa tuwekeze sasa kwenye michezo. Huu mtindo wa kufanya siasa kwenye timu zetu za Simba na Yanga hausaidii chochote!

Tuache siasa ambazo hazitupeleki mbele. Tuache siasa zisizokuwa na uhakisia. Tunajidanganya bure. Yanga inaweza kufuzu leo Sudan lakini sio kwa maagizo ya waziri. Ni kwa sababu ya maandalizi na uwezo iliyonayo. Tupunguze kuzipa timu zetu presha isiyokuwa na msingi wowote. Kama ikifika mahali klabu zetu zinahitaji msaada wa serikali, basi hapo serikali ijitose kote.

Sio kwenda kwa Yanga tu na Simba pekee, tuwaone pia wanajitokeza kwa timu kama Biashara United, Geita Gold, Azam ama klabu nyingine ambao huziwakilisha taifa letu kimataifa.

Sijapenda maagizo ya waziri, kwani sidhani kama yanasaidia. Sidhani kama huo ndio wajibu wa serikali kwenye kuendeleza michezo.

Chanzo: Mwanaspoti