Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hivi ndivyo vilabu vikubwa vinavyomgombania Mzize wa Yanga

Mzize Kiboko.jpeg Hivi ndivyo vilabu vikubwa vinavyomgombania Mzize wa Yanga

Fri, 23 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yanga SC imezidi kugoma kumuuza Kinda Clement Mzize (20) baada ya Ofa ya Pili kutumwa na Wydad Casablanca yenye thamani ya $200,000 (Tzs 542m) kukiwa na kipengele cha kuongezeka hadi $500,000 (Tzs 1.4b) kutokana na utendaji wake.



Klabu ya Aalborg BK (AaB) inayoshiriki ligi kuu nchini Denmark imetuma ofa kwa mchezaji wa klabu ya Yanga Clement Mzize ofa ya kuipa Yanga Ada ya usajili ya dola 100,000 (Zaidi ya milioni 270 za Kitanzania) huku ikimpa Mzize ofa ya kusaini mkataba wa miaka minne wenye mshahara wa dola 26,000 (zaidi ya milioni 70 za Kitanzania) kwa Mwezi.

-Pia kuna bonasi kwa Mzize iwapo atafanikiwa kucheza kikosi cha kwanza (First Eleven) kwenye michezo ya ligi kuu nchini Denmark (SuperLiga) au michezo ya Ulaya (UEFA Champions League, UEFA Europa League au UEFA Conference League ) katika bonasi hiyo akifanikiwa kuanza kwenye kikosi cha kwanza (First Eleven).

-Michezo 10 mshahara utapanda hadi dola 35,000 (zaidi ya milioni 94 za Kitanzania)

-Michezo 20 mshahara utapanda hadi dola 45,000 (Zaidi ya milioni 121 za Kitanzania)

-Michezo 30 mshahara utapanda hadi dola 55,000 (Zaidi ya milioni 149 za Kitanzania)

-Michezo 40 mshahara utapanda hadi dola 65,000 (Zaidi ya milioni 176 za Kitanzania)

-Michezo 50 mshahara utapanda hadi dola 75,000 (Zaidi ya milioni 203 za Kitanzania) kwa Mwezi.



Kaizer Chiefs ya Nabi nayo imetuma ofa ya kumtaka Mzize huyo huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live