Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hivi ndivyo pisi kali ya Ronaldo inavyopiga hela

Ronaldo Rodriguez Hivi ndivyo pisi kali ya Ronaldo inavyopiga hela

Mon, 3 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Utajiri wa supastaa Cristiano Ronaldo unaripotiwa kuwa Dola 600 milioni.Ni mkwanja mrefu kweli kweli. Lakini, ushawahi kujiuliza, mwanamke, ambaye Ronaldo amezama penzini kwake, atakuwa anaishi maisha matamu kiasi gani? Unadhani atakuwa anaomba na ya kutolea?

Sasa ni hivi, Ronaldo baada ya kupita kwa wanawake kibao, amekwenda kunasa kwa mrembo wa Kihispaniola, mzaliwa wa Argentina, Georgina Rodriguez.

Georgina alizaliwa Januari 27, 1994 huko Buenos Aires, Argentina. Na kwa taarifa tu, kama hufahamu, mrembo Georgi-na, hategemei sana pesa za mpenzi wake, Ronaldo - kwani hata yeye mwenyewe, anamiliki mkwanja mrefu tu, anabadili-sha mboga. Mrembo huyo anaripotiwa kuwa na pato linalofikia Dola 10 milioni.

GEORGINA ANAPIGAJE PESA?

Mrembo Georgina kazi yake ni mwanamitindo. Amekuwa akipiga pesa pia kupitia vipindi vyake kadhaa vya televisheni, huku akipiga pia mkwanja kupitia matangazo ya kibiashara yanayokea kwenye mtandao wake wa Instagram wenye wa-fuasi zaidi ya milioni saba. Mrembo Georgina amekuwa akipamba pia kurasa za mbele za majarida maarufu duniani.

Mama yake Georgina ni Ana na baba yake ni Jorge, ambaye alikuwa kocha wa timu ya soka ya Jacetano. Mwanzoni Georgina alikuwa akijifunza kudansi muziki na baadaye alikuwa akifanya kazi ya uhudumu.

Mrembo Georgina alipohamia mji wa pwani wa San Sebastian, ndiko alikoanza kufanya mambo ya mitindo kwenye du-ka la Massimo Dutti. Baadaye Georgina alikwenda kuwa muuzaji msaidizi kwenye duka la Gucci huko Madrid.

MAHABA NA CRISTIANO RONALDO

Georgina alianza kuwa maarufu mwaka 2016 wakati alipokutana na mwanasoka Ronaldo, ambaye kwa wakati huo alikuwa akikipiga Real Madrid.

Kila kitu kilikuwa wazi baada ya kuonekana wakiwa wameshikana mikono huko Disneyland Paris. Wakati wanakutana, mrembo Georgina alikuwa akifanya kazi kwenye duka la Gucci huko Madrid. Kilichoelezwa ni baada ya mrembo Georgina kumwona Ronaldo alianza kutetemeka na kilichofuatia baada ya hapo, wawili hao tayari wana watoto pamoja.

Novemba 2017, walifanikiwa kupata mtoto wao wa kwanza, binti Alana Martina. Na miaka minne baadaye, Ronaldo na Georgina walipata pacha, ambapo hata ovyo mmoja alifariki dunia.

Lakini, kabla ya hapo, Ronaldo tayari alikuwa na watoto watatu kutoka kwa mama wasiojulikana.

Wakati mwingine mrembo Georgina amekuwa akijitutumua na kumnunulia zawadi ikiwamo magari kwa ajili ya shereke za za siku za kuzaliwa mpenzi wake, lakini ukweli ni pesa anayomiliki mrembo huyo ni kama kitone tu kwenye bahari mbele ya mkwanja wa Ronaldo.

MAKAZI NA USAFIRI

Mrembo Georgina kwa kuwa tu kwenye mahaba na Ronaldo anapata muda wa kuishi kwenye majumba ya maana kabisa yanayomilikiwa na mpenzi wake kuanzia Madrid, Ureno, Marekani na England. Kuhusu usafiri, mrembo Georgina atakuwa anawatambia tu warembo wenzake kutokana na kubadili gari kwa kadri anavyotaka, huku familia hiyo pia ikiwa na ndege na boti za kifahari.

Chanzo: Mwanaspoti