Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hivi ndivyo kanuni ilivyowabeba Yanga kupenya Robo Fainali CAF

Yanga Bilioni 2 CAF Hivi ndivyo kanuni ilivyowabeba Yanga kupenya Robo Fainali

Mon, 26 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kumekuwa na maswali mengi kwa watu wakijiuliza inawezekana vipi Yanga kuvuka hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa afrika hali ya kuwa kuna mzunguko wa mchezo mmoja umebaki na mpinzani wake wa karibu CR Belouizdad ana uwezo wa kufikisha alama kama za Yanga (8) na kumpiku idadi ya magoli?

Sasa ipo hivi, baada ya Yanga kushinda magoli 4-0 dhidi ya Belouizdad juzi Jumamosi kwa Mkapa Yanga imeweza kufikisha Point 8 kukaa nafasi ya pili katika kundi lake na Kwa matokeo haya Yanga imeungana na Al Alhy kuingia moja kwa moja Robo Final ya CAF Champions league kabla ya mechi baina yao hao hao Weekend ijayo Jiji Cairo Egypt.

Kikanuni Yanga haihitaji tena kitu chochote katika mchezo wa mwisho dhidi ya Al Alhy zaidi ya kama watashinda wanakuwa Washindi wa Kwanza wa kundi basi.

KANUNI ZINAWABEBAJE YANGA

Mchezo wa Kwanza Cr Belouizdad 3 - 0 Yanga na Mchezo wa Leo wa pili Yanga 4 - 0 Belouizdad hii ina maana katika Head 2 Head kuwa Yanga wamewazidi Belouizdad kwa goli moja hivyo hata CR BELOUIZDAD washinde mchezo wa mwisho wanafikisha Point 8 ambazo Yanga Tayari anazo ila hata afunge magoli mangapi hawezi kuwa juu ya Yanga hivyo ndio utaratibu unavyombeba Yanga kwenda Robo Fainali.

UTARATIBU WA DROO

Droo ya kupanga Michezo ya Robo Fainali itachezeshwa Mwezi Machi katikati ili kujua Kila timu inacheza na nani kwa kufuata yafuatayo:

1. Timu za kundi moja haziwezi kukutana

2. Timu zote mshindi wa pili kwenye Kundi zitaanzia nyumbani

3. Kila timu itapangiwa mpinzani mmoja kati ya Watatu waliopo

Kutokana na Utaratibu huu ina maana Yanga anaweza kupangiwa kati ya Timu hizi Petro Atletico de Luanda ya Angola, Asec Mimosa ya Ivory Coast na Mamelod Sundown/ TP Mazembe hii itategemea matokeo yao ya mchezo wa mwisho South Africa wanacheza wenyewe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live