Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hivi ndivyo Yanga ilivyosepa na milioni 15 za Rais Samia

PESA YANGA.jpeg Hivi ndivyo Yanga ilivyosepa na milioni 15 za Rais Samia

Mon, 20 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga imefanikiwa kuondoka na alama tatu mbele ya timu ya TP MAzembe ya nchini DR Congo baada ya kuichapa kwa mabao 2-1 kwenye dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Baada ya ushindi huo, Yanga wamefanikiwa kubeba tsh milioni 15 walizokuwa wameahidiwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa kila bao watakalofunga watapewa Tsh milioni 5, hivyo kwa mabao matatu ni sawa na Sth milioni 15.

Pesa hizo taslim zimekabidhiwa na Waziri wa Michezo, Pindi Chana akishirikiana na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa mara tu baada ya mchezo huo kumalizika.

Yanga katika mchezo huo waliweza kutawala katika kipindi cha kwanza ambapo walifanikiwa kupata mabao mawili ya haraka kupitia kwa nyota wao Kennedy Musonda dakika 7 na Mudathir Yahaya kufunga dakika ya 11.

Kipindi cha pili Yanga walirudi wakiwa wanajiamini hivyo kuwafanya TP Mazembe wachezee mpira na kufanikiwa kupata bao kupitia kwa Alex Ngonga aliepiga mpira wa adhabu na kutinga nyavuni.

Bao la tatu limefungwa na Tusila Kisinda dakika ya 91 ya mchezo baada ya kuingia akitokea benchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live