Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hivi ndivyo Singida walivyotoboa Nusu Fainali Azam Sports Federation

Hans Van Pluijm Singida Kocha Mkuu wa Singida Big Stars (SBS), Hans Van Pluijm

Wed, 5 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Singida Big Stars (SBS), Hans Van Pluijm ametaja siri ya kuibuka na ushindi mnono katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Mbeya City.

Katika mchezo huo ulifanyika juzi katika Uwanja wa Liti mkoani Singida, SBS iliibuka na ushindi wa mabao 4-1, mabao ya Bruno Gomes dakika za 7 na 57, Bright Adjei na Francy Kazadi dakika za 10 na 27.

Bao la kufutia machozi la Mbeya City lilifungwa na mshabuliaji Eliud Ambokile dakika ya 55 ambaye aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Juma Shemvuni.

SBS itasubiri mshindi kati ya Yanga na Geita ambazo zinacheza Aprili 8 mwaka huu katika Uwanja wa Azam Complex Chamanzi, jijini Dar es Salaam.

Timu hiyo iliweka kambi ya siku nane (8) jijini hapa kujiandaa na mchezo huo, ilicheza michezo ya kirafiki na Dodoma Jiji na timu ya vijana U20 ya Dodoma Jiji.

“Nafikiri tulijandaa vizuri tuliweka kambi Dodoma, tulifanya maandalizi mazuri tukiwa kule na leo tumecheza vizuri tumeweza kupata matokeo mazuri,” alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live