Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hivi ndivyo Saido anavyowaburuza Chama, Mayele Ligi Kuu

Saidoo Simba Saido Ntibazonkiza

Sun, 5 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji wa klabu ya Simba Saidoo Ntibazonkiza amefanikiwa kua kinara katika orodha ya wachezaji waliohusika kwenye magoli mengi kwenye ligi kuu ya NBC msimu huu mpaka sasa.

Ntibazonkiza ndio kinara anaengoza kwa kuhusika kwenye magoli mengi kwa maana ya magoli aliyoyafunga pamoja na pasi za mabao ambazo tayari amepiga mpaka sasa, Kiungo huyo hatari tayari ameshaweka kimiani mabao 10 katika ligi kuu ya NBC huku akifanikiwa kupiga basi 8 za mabao hivo kahusika kwenye jumla ya mabao 18.

Kiungo huyo amefanikiwa kufikisha idadi hiyo ya namba akivitumikia vilabu viwili ndani ya ligi kuu ya NBC kwani mchezaji huyo kacheza nusu msimu katika klabu ya Geita Gold, Huku dirisha dogo la usajili akijiunga na klabu ya soka ya Simba.

Saidoo Ntibazonkiza amekua kwenye kiwango bora msimu huu huku akiendeleza moto alioanza kuuwasha ndani ya Geita ukihamia klabu ya Simba ambayo anaitumikia mpaka sasa, Mchezaji huyo amekua kileleni kwenye kuhusika kwa mabao akifuatiwa na mchezaji mwenzake wa klabu ya Simba Clatous Chama.

Ntibazonkiza akiwa amehusika kwenye mabao 18 mwamba wa Lusaka Clatous Chama yeye amehusika kwenye mabao 17 mpaka sasa akipiga pasi 14 za mabao na kufunga mabao matatu mpaka sasa hivo jumla ni mabao 17, mchezaji mwingine aliehusika kwa mabao mengi ni Fiston Mayele aliefunga mabao 15 na kupiga pasi moja ya bao na kuhusika kwenye mabao 16 ya ligi kuu ya NBC.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live