Wed, 8 Feb 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Jina la kiungo wa Manchester United, Casemiro limekosewa kuandikwa na kutamkwa kwa muda mrefu, lakini Mchezaji mwenyewe ameacha iwe hivyo akiamini kukosewa kwa jina kunamfanya acheze vizuri uwanjani.
Anasema “Nilipoanza kucheza Soka Sao Paulo, kuna Mechi walikosea kuandika jina langu kwenye jezi, iliwekwa ‘E’ badala ya ‘I’, nilicheza vizuri sana mechi hiyo.
Baada ya Mchezo kumalizika nikaijulisha Klabu isirekebishe kosa hilo, tangu hapo Jina limeendelea kukosewa hadi sasa. Jina langu halisi ni Carlos Henrique Casimiro na sio Casemiro.”
Chanzo: www.tanzaniaweb.live