Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hivi ndivyo Gary Neville anavyowapiga Manchester United

Neville Pic Gary Neville

Wed, 5 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Garry Neville ni moja ya watu wawili ninawaopenda sana kuwasikiliza linapokuja suala la uchambuzi ligi kuu ya England.

Linapokuja suala la Liverpool napenda sana kumsikia Jammie Caragher, linapokuja suala la Manchester United napenda sana kumsikiliza Garry Neville.

Wikiendi iliyopita nikatega tena sikio langu kusikia maoni ya Garry Neville juu ya kipigo cha Manchester United.

Garry Neville alikumbushia maoni yake alioyatoa juu ya United wiki tatu zilizopita kwamba, Manchester United itakapoanza kucheza dhidi ya timu 10 za juu, itaanza kuteseka. United ina tabia ya kuteseka inapokutana na timu zilizopangika vizuri.

Kwa maelezo ya Garry Neville ni kwamba, Manchester United ni kati ya timu zisizo na mpangalio kabisa uwanjani. Wakiwa na mpira, wakiwa hawana mpira, wakilinda na wakishambulia wanakuwa hovyo sana.

Zaidi ya hilo, staili wanayocheza Manchester United na kikosi kinachopangwa kwenda kutekeleza majukumu havina uwiano. Neville anasema asingekubali kuwa beki timu yenye Sancho, Ronaldo, Pogba, Bruno na Greenwood ndani kwa pamoja.

Manchester United haina watu ambayo yeye anawaita ‘work horses’. Work horses kama Tom Cleverley Ji Sung Park na Nicky Butt.

Lakini pia Neville amewamwagia lawama wachezaji wakubwa wa United kwamba hawajitumi. “Ukiwa world class, inabidi uoneshe kuwa wewe ni world class. Jitume hata timu inapopotea hakikisha unaonesha tofauti” Ndani ya United, Neville hamuoni mchezaji anayejituma kama KDB, Sadio Mane, Bernardo Silva au Ngolo Kante.

Binafsi yangu, Nimekubaliana sana na mawazo Neville. Tabu tu ni kutokumuongelea Solksjaer. Licha ya kasoro nyingi anazoziona ndani ya United, Bado yeye haoni shida ya Ole Gunner Solksjaer.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live