Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hivi hapa viingilio Simba SC Vs ASEC Mimosas

Hivi Hapa Viingilio Simba SC Vs ASEC Mimosas.jpeg Hivi hapa viingilio Simba SC Vs ASEC Mimosas

Thu, 16 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, ametaja viingilio vya mchezo wao wa kwanza wa hatua ya Makundi dhidi ya ASEC Mimosas utakaopigwa Novemba 25, 2023.

Ahmed ameyasema hayo leo Novemba 16, 2023 alipokuwa akitangaza ratiba yao kuelekea mchezo huo mkubwa utakaopihgwa kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar.

“Leo tunazungumzia maandalizi ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas. Utachezwa siku ya Novemba 25, 2023 saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Mkapa. Wageni watawasili Novemba 23, 2023 wakiwa na msafara wa watu 31. Waamuzi wa mchezo watatoka nchini Misri.”

“Viingilio vya mchezo huu ni; Mzunguko - Tsh. 5,000. VIP C - Tsh. 10,000. VIP B - Tsh. 20,000. VIP A - Tsh. 30,000 Platinum - Tsh. 150,000.”

“Kikosi kipo mazoezini kuanzia siku ya Jumatatu. Mazoezi yanawahusu wachezaji wote ambao hawana majukumu ya timu za taifa. Ambao wapo kwenye timu za taifa watajiunga na wenzao wakitoka huko. Kikosi bado kipo chini ya Kocha Seleman Matola na Dani Cadena. Uongozi unaendelea na jitihada za kutafuta kocha mpya, mchakato utakamilika muda si mrefu.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live