HATIMAYE dili la mshambuliaji Jean Marc Makusu kutua Yanga limeingiwa na doa mara baada ya uongozi wa timu hiyo kugundua kuwa mshambuliaji huyo kuwa na majerahaya mara kwa mara.
Hapo awali uongozi wa Yanga ulikuwa katika mpango wa kumsajili Makusu kwa ajili ya kuja kuongoza nguvu katika eneo la ushambuliaji ya timu hiyo ambapo kwa sasa linachezwa na Fiston Mayele na Heritier Makambo.
Chanzo cha ndani kutoka Yanga kimesema kuwa uongozi wa Yanga umeamua kuachana na Makusu kutokana na mshambuliaji huyo kuwa na majeraha ya mara kwa mara mara baada ya kuwahi kuvunjika mguu wake wa kushoto kipindi ambacho yupo Orlando Pirates ya Afrika Kusini.
“Uongozi wa Yanga umeona ni busara kwao kuachana na usajili wa Makusu kutokana na majeraha ambayo amekuwa akipata mara kwa mara baada ya kuwahi kuvunjika mguu alipokuwa akikipiga Orlando Pitares.
“Tangu avunjike mguu wake wa kushoto na alipopona bado alikuwa akipata majeraha ya mara kwa mara tofauti na alipokuwa AS Vita ambao alikuwa yupo fiti na alikuwa anacheza kwa kiwango kikubwa sana, hivyo ni ngumu tena kwake kusajiliwa na Yanga mara baada ya kugundua hilo,” kiliweka wazi chanzo hicho.
Makusu mwenyewe amefunguka: “Kila kitu kuhusu usajili wangu uongozi wangu ndio unahusika, mambo ya usajili huwa yana mambo mengi kwangu nacheza mpira kisha uongozi unatenda zaidi juu ya usimamizi wangu.”