Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hitimana presha imepanda lala salama

Hitimana Pic Data Hitimana presha imepanda lala salama

Sun, 28 Feb 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Clezencia TryphoneMore by this Author USHINDANI mkubwa uliopo kwa sasa kwenye mechi za lala salama Ligi Kuu Bara unaonekana kumpa presha Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Hitimana Thiery.

Hitimana alijiunga Mtibwa Sugar akitokea Namungo baada ya kushindwana kimaslahi katika kuongeza mkataba wa kuendelea kukinoa kikosi hicho.

Akizungumza na Mwanaspoti Online, Hitimana amesema, ushindani ni mkubwa kwani kila timu wanayokutana nayo inapambana kujinasua kushuka na kusalia kwenye ligi hiyo.

Amesema kutokana na hilo ndiyo sababu inayofanya ushindani uongezeke hivyo kila timu inatakiwa kuhakikisha inapambana kupata matokeo.

"Ligi ni ngumu kwa sasa ushindani ni mkubwa sana kwa kila timu, ila kama kocha najitahidi kuzungumza na vijana wangu wajitahidi kupambana kila tunapokuwa na mechi iwe ya ndani au ya ugenini," amesema.

Hitimana amesema, kulingana na ugeni aliokuwa nao kwa sasa ndani ya timu hiyo kuhakikisha timu inasalia kwenye ligi kwani nafasi iliyopo hairidhishi.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz