Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hitimana atajwa JKT

KMC  Thierry Hitimana Hitimana atajwa JKT

Thu, 11 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kufanikiwa kurejesha timu Ligi Kuu Tanzania Bara kuelekea msimu mpya wa 2023/24, uongozi wa Klabu ya JKT Tanzania upo katika mchakato wa kumpa ajira, aliyekuwa Kocha Mkuu wa KMC FC, Thierry Hitimana, kukinoa kikosi hicho kwa msimu ujao, imefahamika.

Licha ya uongozi wa JKT Tanzania kutoweka wazi suala hilo huku wakidai kuwa wataendelea na Kocha Hamsini Malale aliyeipandisha timu hiyo Ligi Kuu endapo anahitaji kuendelea kubaki katika timu hiyo, lakini taarifa za ndani zimedokeza kuwa klabu hiyo ipo katika mazungumzo na Hitimana.

Hata hivyo, Malale alipoulizwa juu ya mustakbali wake juu ya maboresho ya kikosi chake, alisema hawezi kuweka mipango yake ya usajili ya msimu ujao kwa sababu hajui hatima yake.

Alipotafutwa Hitimana mwenyewe akagoma kuweka wazi dili hilo akisisitiza kuwa hakuna timu iliyomfuata.

"Hakuna kiongozi aliyenifuata kwa ajili ya mazungumzo yoyote, hilo suala kama lipo, kwangu ni vizuri kwa sababu hakuna mtu anayekataa kazi anapoipata," alisema Hitimana.

Hitimana ni kocha mwenye uzoefu wa Ligi kuu ya Tanzania Bara akiwa amewahi kuzifundisha Namungo Fc na Simba kabla ya kujiunga na KMC.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: