Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hitimana amrithi Gomes

HITIMANA Thiery Hitimana, Kocha mkuu wa Simba

Tue, 26 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa Kocha msaidizi wa Klabu ya Simba SC, Thierry Hitimana amekuwa Kocha Mkuu wa Simba katika kipindi hiki cha mpito akisaidiwa na Selemani Matola.

Hitimana anakamata nafasi hiyo baada ya Simba kuachana na Kocha Mkuu M-faransa Didier Gomes Da Rosa.

Gomez aliajiriwa Simba SC msimu uliopita kuchukua nafasi ya Sven Vandebroek ambaye aliachana na Simba SC kwa madai ya majukumu ya kifamilia lakini baadae akaibukia klabu ya FAR RABAT ya Morocco.

Kwenye Ligi ya nyumbani aliiongoza Simba kushinda Ligi Kuu kwa mara ya 4 mfululizo na Kombe la FA mara ya pili mtawalia.

Simba imetwaa vikombe 4 na makocha tofauti tofauti Pierre Lechante, Patrick Aussems, Sven Vandebroke na Didier Gomez.

Gomez pia aliibuka Kocha bora wa msimu wa Ligi Kuu kwenye tuzo za TFF ambazo zilitawaliwa na Simba SC zilizofanyika tarehe 21.10.2021.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live