Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hitimana akiri kazi nzito Simba

HITIMANA Hitimana akiri kazi nzito Simba

Fri, 29 Oct 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Dar es Salaam. Simba inatakiwa kufanya kazi kubwa kurejesha ubora wao, huku kaimu kocha mkuu wa kikosi hicho, Hitimana Thiery akisema ana kazi ya kurejesha morali ya nyota wake kwa sasa.

Simba iliondoshwa katika Ligi ya Mabingwa Afrika Jwaneng Galaxy Oktoba 24 Uwanja wa Mkapa, baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-1 na kuondolewa kwa jumla ya mabao 3-3 baada ya mchezo wa awali kushinda ugenini mabao 2-0.

Hitimana alisema kikosi chake ni kizuri, lakini nyota wake wanahitaji kurejeshwa mchezoni baada ya matokeo mabaya yaliyopita.

“Nina kazi ya kuwafanya vijana wangu warudi mchezoni, maana matokeo ya Galaxy yamewatoa kabisa mchezoni, hata mimi kocha niliumizwa sana na matokeo hayo,” alisema Hitimana.

Aidha Hitimana alisema, mbali na matokeo hayo hata kuondolewa kwa benchi kocha mkuu Didier Gomes na wenzake nayo imechangia wachezaji kuwa na presha kubwa.

Kuhusu mchezo wa juzi dhidi ya Polisi Tanzania, Hitimana alisema kikubwa alimshukuru Mungu kwa kupata pointi tatu licha ya wachezaji wake kuwa na presha kubwa na kutocheza vizuri.

Related Gomes atoa onyo kali, ampa neno Mkude



EXCLUSIVE: Gomes afunguka.. kuna watu wameonewa


Simba yaipandisha Yanga kileleni


Hitimana anaanza hivi Simba“Leo (juzi) tumecheza kwa presha kubwa, mchezo huu kulikuwa na wapinzani, wawili wa kwanza ni sisi wenyewe na wa pili Polisi,” alisema Hitimana.

Katika mchezo wa juzi, Hitimana aliwaanzisha kikosini wachezaji wanne wapya tofauti na mchezo uliopita, ambao ni Joash Onyango, Erasto Nyoni, Kibu Denis na Meddie Kagere.

“Thadeo (Lwanga) ni majeruhi na hata Jonas (Mkude) hakuwa fiti asilimia 100 ndiyo maana tumefanya mabadiliko ya kikosi, ingawa nilitamani kuanza na washambuliaji wawili, lakini kikubwa tunafurahi kwa ushindi,” alisema Hitimana.

Mdau wa kabumbu Tigana Lukinja alisema, Simba ina kikosi kizuri huku akimtaka kocha kujitahidi kuwarejesha mchezoni kwa kuwa yaliyopita yamepiga sasa wanaganga yajayo.

“Simba inatakiwa kujipanga. Bado mashabiki wa klabu hiyo hawajaridhishwa na kiwango kinachoendelea kuonyeshwa na Simba, jambo ambalo linawapa mawazo,” alisema.

Kiwango na matokeo katika mechi tano zilizopita za Simba zikiwemo mbili za kimataifa zinaonyesha jinsi kikosi hicho kilivyo na kazi kubwa ya kufanya msimu huu.

Simba ilianza ligi kwa kucheza na Biashara na kutoka suluhu, huku nahodha John Bocco akikosa penalti katika mchezo huo na mechi ya pili ikishinda bao 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji, wakati wapinzani wao wakiwa pungufu baada ya mchezaji wao, Anuary Jabir kuonyeshwa kadi nyekundu.

Ikahamia kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na kuanzia ugenini ilikopata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana, lakini ikachapwa nyumbani 3-1 katika mchezo wa marudiano na kuondolewa mashindanoni.

Simba ilirejea kwenye ligi na kuichapa Polisi Tanzania kwa bao la penalti lililofungwa na Rally Bwalya.

Mmoja ya makocha wazoefu nchini, Mrage Kabange alisema bado Simba inaweza kufanya vizuri na kutetea ubingwa wake, lakini kikubwa ni wachezaji kwanza kutuliza akili.

“Wanatengeneza nafasi lakini wanashindwa kuzitumia na inavyoonekana wanacheza katika presha kubwa ya kutafuta matokeo na kurudia mafanikio, jambo hili wasipoliangalia wanaweza kupotea. Watulize akili,” alisema Kabange.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz