Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hitimana akiri kazi ipo

Hitimana Kazi Ngumu Hitimana akiri kazi ipo

Wed, 15 Feb 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Matokeo mabovu kwenye kikosi cha KMC yamemfanya kocha wake, Thierry Hitimana kukiri yupo katika wakati mgumu kukabiliana na michezo minane inayofuata akianza na ule wa Yanga utakaopigwa Februari 22 kwenye Uwanja wa Mkapa.

KMC katika michezo yake mitano iliyopita haijaonja ladha ya ushindi ambapo imepoteza minne na kutoka sare mmoja huku mara ya mwisho kushinda ilikuwa ni ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Polisi Tanzania Desemba 22 mwaka jana.

“Nimekaa na mchezaji mmoja mmoja na kuwaambia hatuna matokeo mazuri na ukiangalia ratiba yetu ni ngumu, hivyo ni wakati wa kila mtu kuonyesha thamani yake kwa kuipambania timu licha ya kukabiliwa na michezo migumu.”

Hitimana aliongeza katika kipindi hiki wakiwa kwenye mchakato wa kutafuta mechi zaidi ya mbili za kirafiki ili kujiweka fiti wakitambua wapinzani wao Yanga wanaendelea kucheza michezo ya CAF itakayowaongezea ari zaidi.

Kwa upande wa kipa wa kikosi hicho, Hussein Abel alisema licha ya ratiba ngumu inayowakabili ila bado wana nafasi ya kufanya vizuri katika michezo iliyobaki na wala hawana mpinzani yoyote ambaye wanamhofia kwa sasa.

“Ili uwe bora ni lazima ushindane na waliokuzidi, tuna mechi ngumu lakini wachezaji tumekaa chini na kuambizana wenyewe kwa wenyewe kwamba huu ni wakati wetu wa kuonyesha tuna uwezo wa kupambana na mpinzani yoyote.”

Wakati kikosi hicho kikikabiliana na Yanga Februari 22 mwaka, kitapumzika siku tatu tu kisha kitarudi uwanani kupambana tena na Azam FC Februari 25 katika mchezo mwingine mkali na mgumu utakaopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Chanzo: Mwanaspoti