Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hitimana: Simba inarudi kwa kasi

Coach Hitimana Thiery Hitimana, Kocha mkuu wa Simba

Sat, 30 Oct 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Kaimu Kocha Mkuu wa Simba, Hitimana Thiery amesema, ana kazi kubwa ya kurejesha morali ya nyota wake mchezoni lakini ana imani kitambo kidogo watarudi kwenye fomu yao na mashabiki watafurahi.

Amesema kitendo cha kuondoshwa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na Kocha Mkuu Didier Gomes kufutwa kazi kimewapa presha lakini ameanza kusuka mikakati ya kudhibiti hali hiyo na kuanza maisha mapya.

Kwa mujibu wa Hitimana ambaye alikuwa mshikaji mkubwa wa Gomes, kikosi chake ni kizuri lakini nyota wake wanahitaji sana kurejeshwa mchezoni baada ya matokeo mabaya yaliyopita.

“Nina kazi ya kuwafanya vijana wangu warudi mchezoni, maana matokeo ya Galaxy wamewatoa kabisa mchezoni hata mimi kocha niliumizwa sana na matokeo hayo.”

Aidha Hitimana amesema, mbali na matokeo hayo hata kuondolewa kwa benchi la ufundi kocha Mkuu Didier Gomes na wenzake na chenyewe kimechangia wachezaji kuwa na presha kubwa.

Kuhusu mchezo wa juzi dhidi ya Polisi Tanzania Hitimana amesema; “Tulicheza kwa presha kubwa sana na mchezo huu kulikuwa na wapinzani wawili wa kwanza sisi wenyewe na wa pili Polisi.”

Juzi Hitimana aliwaanzisha kikosini wachezaji wanne sura mpya tofauti na mchezo uliopita ambao ni Joash Onyango, Erasto Nyoni, Kibu Denis pamoja na Meddie Kagere.

“Thadeo Lwanga ni majeruhi na hata Jonas Mkude hakuwa fiti asilimia 100 ndiyo maana tumefanya mabadiliko yale ya kikosi ingawa nilitamani kuanza na washambuliaji wawili lakini kikubwa tunafurahi kwa ushindi,”amesema Hitimana.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz