Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Historia ya Ghanim Al-Muftah aliyenogesha ufunguzi wa Kombe la Dunia Qatar

Duh Mak Mtoto Historia ya Ghanim Al-Muftah aliyenogesha ufunguzi wa Kombe la Dunia Qatar

Sun, 27 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ni Mjasiriamali anaetengeneza ICE CREAM zenye Hadhi ya NYOTA TANO! Kijana mashuhuri kutoka Qatar aliyeongoza sherehe za Ufunguzi wa Michuano ya Kombe la Dunia 2022.

Ghanim Al-Muftah alizaliwa Mei 5 mwaka 2002. Akiwa ni Mtoto pacha, yeye na Kaka yake.Wakati kaka yake akiwa mzima wa afya, yeye alizaliwa na ugonjwa adimu unaojulikana kama Caudal Regression Syndrome (CDS), Ugonjwa ambao huharibu maendeleo ya mgongo wa chini.

Ghanim Alipewa miaka michache ya kuishi na wataalamu wa afya, wengi wakisema hawezi kuzidi miaka 15, Lakini sasa ana miaka 20, na ni miongoni mwa vijana mashuhuri kutoka Qatar.:Kabla ya kuzaliwa Mama yake alishauriwa, mimba yake itolewe ili kuwaondolea wazazi kadhia na mateso ya kuishi na mtoto mwenye hali adimu ya kiafya Lakini Kwa ujasiri, Wazazi wa Ghanim walipingana na ushauri huo na kukubali kumsaidia wakati wote.

“Nitakuwa mguu wake wa kushoto na wewe utakuwa mguu wake wa kulia”. Mama yake alisema.

Ghanim alipokuwa akikua, aliona vigumu kuhudhuria Shule kwa sababu ya dhihaka na uonevu kutoka kwa Wanafunzi wenzake.

Hata hivyo, Mama yake alimtia moyo kuzungumza na Wanafunzi wenzake kuwafundisha kuhusu hali yake, na kuhamasisha Jamii.

Ghanim Al-Muftah ni miongoni mwa wajasiriamali wadogo zaidi wa Qatar, anayesherehekea mafanikio yake na kupanua biashara yake. Kwa msaada wa wazazi wake, Ghanim alizindua kampuni ya kutengeneza ‘Ice cream’ (Gharissa Ice Cream), kampuni iliyoko Qatar inayotengeneza ICE CREAM Zenye hadhi ya NYOTA TANO!.

Licha ya ulemavu wake, Ghanim anapenda kushiriki katika michezo kama Kuogelea, Kupiga mbizi kwenye barafu, Kandanda, Kupanda mteremko na Kuteleza kwenye barafu.Kwa kushangaza, Ghanim amepanda Jebel Shams, kilele cha mlima mrefu zaidi katika eneo lote la Ghuba. Bila woga, na ametangaza hadharani nia yake ya kupanda Mlima Everest.

Kujihusisha na shughuli hizi za kimichezo na harakati zake za kutetea haki za walemavu, hatimaye alichaguliwa kuwa balozi wa kombe la Dunia huko Qatar 2022.

Katika sherehe za ufunguzi wa kombe la Dunia 2022, alikua pembeni ya Muigizaji mashuhuri wa Marekani MORGAN FREEMAN Alitoa Hotuba iliyogusa mioyo ya wengi ulimwenguni.

Watu mbalimbali walitoa maoni yao kwenye mitandao ya kijamii, wakisifia ujasiri wa kijana huyu.

Hata hivyo, kila mwaka anapatiwa matibabu ya kitaalamu kutoka na hali yake. lakini hilo halijakatisha ndoto zake kwani Al-Muftah analenga kusoma Sayansi ya Siasa katika Chuo Kikuu, kwa lengo la kuwa Waziri Mkuu wa baadaye wa Qatar. HUYU NDIO GHANIM AL-MUFTAH Mjasiriamali anaetengeneza ICE CREAM Zenye Hadhi ya NYOTA TANO.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live