Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hispania yapata kipigo cha kwanza

20709fd92041700b461ec19d7305c9af Hispania yapata kipigo cha kwanza

Thu, 15 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KIEV, Ukraine

TIMU ya taifa ya Hispania baada ya kushindwa kutumia nafasi nyingi za kufunga ilijikuta ikipokea kipigo cha kwanza baada ya kufungwa 1-0 na wenyeji Ukraine katika mchezo wa Ligi ya Mataifa ya Ulaya.

Hicho ni kipigo cha kwanza kwa Hispania katika kipindi cha miaka miwili.

Mshambuliaji wa Leeds, Rodrigo alishindwa kutumia nafasi mbili za wazi kwa kichwa wakati kipa wa Ukraine, Georgi Bushchan akiwachanganya mabingwa hao wa zamani wa dunia katika uwanja ambao walishinda taji la Euro 2012.

Katika mchezo huo, Hispania ilipiga mashuti 21 kwa ujumla, lakini Ukraine walihitaji shuti moja tu kufunga bao na kuondoka na pointi zote tatu katika mchezo huo uliopigwa jijini hapa.

Mchezaji aliyeingia akitokea benchi, Viktor Tsygankov alikimbia na kuiwahi pasi ya mshambuliaji wa West Ham, Andriy Yarmolenko na kupiga mpira uliompita kipa wa Hispania, David de Gea.

Kipa huyo wa Manchester United alikutwa akiwa nje ya eneo lake lilipotokea shambulio la kushtukiza wakati kikosi cha Luis Enrique kilipopoteza mchezo kwa mara ya kwanza tangu walipofungwa na Croatia 3-2 Novemba mwaka 2018.

Sasa wanaoongoza katika Kundi A4 wakiwa mbele kwa pointi moja, wakiwa mbele ya Ukraine na Ujerumani, ambao walitoka sare ya 3-3 na Uswisi.

Karibu mashabiki 15,000 waliruhusiwa kuingia kuangalia mchezo huo wa Ligi ya Mataifa, ambao kiujumla ulitawaliwa na Hispania.

Wageni Hispania walitawala mchezo huo kwa asilimia 72 ya mchezo huo na kumlazimisha Bushchan kuokoa mara nane, lakini mchezaji huyo wa Dynamo Kiev alikuwa katika kiwango cha juu.

Kocha wa Hispania, Luis Enrique alisema: "Namlaumu De Gea tayari amefanya kosa, lawama nyingi zinamuendea yeye…

"Uwezekano wa kila bao unaangukia kwa timu nzima.

"Kwa kweli tulipata nafasi ya kuwaua mapema kabisa. Ni mchezo tulioutawala, pamoja na Adama Traore tulitengeneza nafasi kibao pale alipopanda juu kushambuliaji.”

Chanzo: habarileo.co.tz