Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hisa za Manchester United zashuka baada ya ripoti kuwa ununuzi umefutwa

Hisa Za Manchester United Zashuka Baada Ya Ripoti Kuwa Ununuzi Umefutwa Hisa za Manchester United zashuka baada ya ripoti kuwa ununuzi umefutwa

Wed, 6 Sep 2023 Chanzo: Bbc

Hisa za Manchester United zimeshuka siku moja baada ya ripoti kuwa wamiliki wa timu hiyo Marekani wataiondoa sokoni.

Hisa za klabu hiyo zilishuka kwa zaidi ya 18% jijini New York siku ya Jumanne.

Hayo yaliwadia baada ya barua pepe iliyotumwa kusema kwamba hakuna mnunuzi aliyefikia bei iliyowekwa ya kuinunua.

Familia ya Glazer yenye makao yake nchini Marekani ilitangaza mnamo Novemba kuwa inafikiria kuuza klabu hiyo ya Ligi ya Premia huku wakitafuta "njia mbadala za kimkakati".

Wenyeviti wenza wa Manchester United, kaka Joel na Avram Glazer, wametoa ofa ya pauni bilioni 10, kulingana na ujumbe uliotumwa kupitia barua pepe.

Hata hivyo, wanunuzi watarajiwa Sheikh Jassim wa Qatar na bilionea wa Uingereza Sir Jim Ratcliffe hawakukaribia kutoa kiasi hicho, gazeti hilo lilisema.

Gazeti hilo lilinukuu chanzo chenye uhusiano wa karibu wa muda mrefu na wamiliki wa klabu hiyo kikisema familia ya Glazer huenda ikajaribu tena mwakani kuiuza klabu hiyo wakati wakitarajia kuvutia wanunuzi wengi zaidi.

Klabu hiyo haikujibu mara moja ombi la BBC la kutoa maoni.

Kushuka kwa bei ya hisa Jumanne kuliondoa takriban $700m (£556m) kutoka kwa hesabu ya soko la hisa la Manchester United.

Sasa ina thamani ya takriban $3.2bn.

Familia ya Glazer ilinunua Manchester United mwaka 2005 kwa $790m.

Hata hivyo, wamekumbana na upinzani mkali kutoka kwa baadhi ya mashabiki wanaowatuhumu kwa kuilimbikizia klabu hiyo madeni na kutowekeza vya kutosha.

Tangu wainunue, klabu hiyo imetumia zaidi ya £1bn kwa malipo ya riba na mkopo, pamoja na gawio la hisa - nyingi zikiwa zimeelekezwa kwa familia ya Glazer.

Lakini klabu hiyo pia imetumia kiasi cha euro 1.36bn (£1.18bn) kwa shughuli za uhamisho chini ya Glazer, huku Manchester City pekee wakiwa na idadi kubwa katika kipindi hicho.

Mwezi uliopita, Kundi la 1958, ambalo linaundwa na mashabiki wanaotaka Glazers kuondoka katika klabu hiyo, lilifanya maandamano huko Old Trafford kuashiria kuendelea kupinga umiliki wa familia hiyo.

Chanzo: Bbc