Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Himid hataki kurudia tena kosa

Wed, 31 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

BAADA ya kushindwa kuibakisha timu yake ya Petrojet, kiungo Himid Mao ameaga klabuni hapo ili kujiunga ENNPI inayoshiriki Ligi Kuu ya Misri, huku akiapa kutotaka kurudia kosa lililomkuta katika klabu yake ya zamani iliyoshuka daraja.

ENNPI ni klabu aliyokuwa akiichezea kwa mkopo winga wa kimataifa wa Tanzania, Shiza Kichuya kutoka Pharco FC inayoshiriki ligi daraja la pili nchini humo.

Himid katika msimu uliopita alikuwa katika uhusiano mzuri wa kuanza katika kikosi hicho, hata hivyo alishindwa kuipigania timu yake kubaki Ligi Kuu.

Himid alisema ni muda sahihi wa yeye kuondoka katika timu hiyo na kwenda kujaribu changamoto katika klabu mpya huku akibainisha kuwa mipango yake ni kuisaidia timu hiyo kufanya vizuri ikiwezekana iweze kuwa na jina kubwa kupitia yeye.

"Ni kweli hiyo timu pia haikuwa na msimu mzuri lakini imefanikiwa kubaki Ligi Kuu ni muda wangu kushirikiana na nyota wengine niliowakuta katika timu hiyo tuweze kuitoa katika nafasi moja kwenda nyingine, sitaki yaliyotokea Petrojet kurudia hapa," alisema.

***

Chanzo: mwananchi.co.tz