Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Himid amrahisishia kazi Salamba

Salama Adam Himid amrahisishia kazi Salamba

Tue, 8 Nov 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Straik mpya wa Ghaz El Mahalla ya Misri, Mtanzania, Adam Salamba amesema kukutana na Himid Mao kwenye timu hiyo, kumempa urahisi wa kuzoea mazingira ya kufanya kazi na kujua namna ya kuendana na wachezaji wengine.

Salamba, aliyewahi kung’ara akiwa na Lipuli na Simba anasubiri ITC kutoka JS Saoura ya Algeria, alisema Himid amempa uzoefu wa namna ya kufanikiwa kucheza kwa kiwango soka la Misri, ingawa alisisitiza kubwa zaidi kwake ni bidii.

“Hakuna kitu kizuri kukutana na Mtanzania mwenzako nchi za watu, Himid ana uzoefu na mji huu, hivyo amekuwa akinielekeza jinsi mazingira yalivyo, jambo ambalo limenifanya nijione mwenyeji,” alisema Salamba aliyezichezea pia Stand United na Namungo na kuongeza;

“Ingawa kitu pekee kitakachokufanya wachezaji wengine wakufahamu zaidi ni kile utakachokionyesha uwanjani, pamoja na kupewa msaada nina jukumu la kupambana kuhakikisha naonyesha uwezo wangu.”

Salamba alisema kwake ni mwiko kukata tamaa, hiyo ndio sababu inayomfanya kupambana kusaka nafasi za kucheza nje bila kuchoka, akizipigania ndoto zake za kucheza soka kwa mafanikio ya juu.

“Najua nilipotoka, najua ninachokitaka, labda niwaambie wachezaji wenzangu wasiruhusu kukata tamaa ili mladi wapo hai, ipo siku watakuja kuishi kile wanachokitafuta kwa muda mrefu,” alisema.

Chanzo: Mwanaspoti