Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Himid amkubali Fiston, asema ni zaidi ya jembe!

Fiston Pic Data Himid amkubali Fiston, asema ni zaidi ya jembe!

Thu, 4 Feb 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

WAKATI mashabiki wa Yanga, wakisubiri kwa hamu kuona mavitu ya mchezaji wao mpya wa kimataifa wa Burundi, Fiston AbdulRazak, Mtanzania aliyecheza naye kikosi kimoja nchini Misri, Himid Mao ‘Ninja’ anaamini mshambuliaji huyo wa kati anaweza kung’ara Ligi Kuu Bara.

Fiston ni kati ya maingizo mpya ndani ya Yanga kupitia dirisha dogo la usajili lililofungwa mwezi uliopita kuiimarisha safu ya ushambuliaji iliyosuasua kwenye duru la kwanza na Himid aliyecheza naye katika timu ya ENPPI iliyopo Ligi Kuu ya Misri amedai jamaa ni zaidi ya jembe,

Himid alicheza na Fiston kwa mwaka mmoja kila mmoja dirisha hilo kuhamia kwingine na alisema ni mshambuliaji mzuri, na kwa namna anavyolifahamu soka la Tanzania anaweza kufanya vizuri licha ya kukabiliwa na presha kubwa kutoka kwa mashabiki wa timu hiyo.

“Ni mshambuliaji mzuri sana, tumekaa pamoja vizuri na uwezo wake naujua, anaweza kuisaidia Yanga kufikia malengo yake, ni mzuri kama atacheza na viungo wenye uwezo wa kutengeneza nafasi, kwa kifupi ni mfungaji, kwa vile anajua kutumia nafasi kwa namna anavyojipanga uwanjani,” alisema.

Himid alisema kama Yanga itamtumia vizuri anaweza kuleta matokeo chanya kikosini hasa baada ya kusikia pia wanaye mshambuliaji mwingine mkali kutoka Burundi, Saido Ntibazonkiza ambao wanafahamiana ndani ya timu ya taifa ya Burundi.

Ndani ya kikosi cha ENPPI walipocheza pamoja, Himid alikuwa akipata nafasi kubwa ya kucheza kulinganisha na Fiston kwani alikuwa akikabiliwa na changamoto ya namba na kuondoka kwake kulitoa nafasi kwa Mnigeria John Ebuka kuingia kikosini.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz