Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Himid achukua nafasi ya Kichuya Misri

69001 Himidi+picha

Wed, 31 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

KIUNGO Himid Mao amejiunga na klabu ya ENNPI  inayoshiriki Ligi Kuu Misri kwa mkataba wa miaka miwili akitokea klabu ya Petrojet iliyoshukaa daraja.

ENNPI ni klabu ambayo winga Shiza Kichuya alikuwa anaichezea kwa mkopo akitokea Pharco inayoshiriki Ligi Daraja la Pili nchini Misri.

Hata hivyo, baada ya mkopo huo kumalizika Kichuya yupo nchini akisubiri kuona namna ambavyo anaweza kupata timu nyingine kwa ajili ya msimu ujao.

Himid, msimu uliopita alikuwa katika kiwango kizuri ndani ya kikosi cha kwanza, hata hivyo alishindwa kuipigania timu yake kubaki Ligi Kuu.

Mratibu wa Kampuni ya Siyavuma Sports Group, Michael Mwebe alisema mchezaji huyo ametua katika kikosi hicho baada ya mazungumzo ya pande mbili kwenda vizuri.

"Ni kweli amejiunga na ENNPI baada ya mazungumzo kwenda vizuri, Himid ni mchezaji mzuri tunaamini kabisa atazidi kufanya vizuri katika Ligi ya Misri," alisema.

Chanzo: mwananchi.co.tz