Nyota wa Tanzania Himid Mao ambaye anaitumikia klabu ya Ghazi El Mahalla ya Misri amefunguka siri ya kuvaa soksi fupi badala ya zile ndefu awapo dimbani kama alivyozoeleka huko nyuma.
Himid amesema ni Ushauri kutoka kwa daktari kuvaa soksi fupi kwani alikuwa akipata Cramps mara kwa mara lakini na tangu aanze kufanya hivyo hali hiyo haimtokei tena.
Himid ni kati ya nyota wa kutumainiwa na kikosi cha Ghazi kinachoshiriki ligi kuu ya Misri na amekuwa chaguo la kwanza la Mwalimu kwenye michezo mingi.
Huu ni mwaka wake wa sita kwenye ardhi ya Misri ambapo amevitumikia vilabu vya Petrojet,Ennpi,Entag El Harby na El Mahala.