Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hilo tizi la Man United ni balaa

Sancho X United Hilo tizi la Man United ni balaa

Wed, 31 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kiungo wa Manchester United na timu ya taifa ya Denmark, Christian Eriksen anaamini timu hiyo inapata tizi la uhakika katika maandalizi ya msimu ujao tofauti na ilivyokuwa uliopita ambapo walifanya maandalizi kama sehemu ya biashara jambo lililowagharimu kwenye mashindano.

Man United ambayo ilianza mazoezi Marekani ambako ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Arsenal katika Uwanja wa SoFi Stadium wikiendi iliyopita kabla ya kusafiri kwenda San Diego ambapo itacheza na Real Betis leo, baada ya hapo hapo itasafiri kwenda South Carolina ambako itacheza na Liverpool.

Katika msimu uliopita mambo yalikuwa tofauti ambapo timu hiyo hadi kufikia sasa ilikuwa imeshafanya safari nyingi na ndefu ikiwa ni pamoja na ile ya maili 3000 ya kwenda na kurudi Houston, Marekani kucheza na Real Madrid.

Msimu huu Eriksen anaamini timu imekuwa makini zaidi katika kupanga ratiba ambayo haiwachoshi wachezaji na imejikita zaidi kuhakikisha inajijenga na siyo kuangalia mambo ya biashara.

"Kwa asilimia mia kuna tofauti kubwa kati ya maandalizi ya msimu uliopita na msimu huu, hususan katika upande wa safiri kwenda katika mechi tofauti na ilivyokuwa msimu uliopita ambapo walizingatia zaidi upande wa wadhamini na eneo la soka na utimamu wa mwili haukupewa kipaumbele," alisema.

Eriksen alisema wakati wa maandalizi mwaka jana walikuwa na safari nyingi ambazo zilikuwa ndefu ilhali msimu huu licha ya kuwa na mambo mengi ya kufanya wamewekewa mazingira rafiki ya safari kutoka eneo moja kwenda jingine na muda wanaotumia kukaa katika ndege sio mwingi, hali inayowapa nafasi nzuri ya miili kuwa sawa.

Eriksen ni mmoja wa wachezaji wa Man United waliopo hadi sasa katika dirisha hili na hakuna timu iliyoripotiwa kuwasilisha ofa kwa ajili ya kumsajili.

Chanzo: Mwanaspoti