Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hilo la dili la Musonda Yanga kufuru, kocha Mzambia ashindwa kujizuia

Musonda Musonda Hilo la dili la Musonda Yanga kufuru, kocha Mzambia ashindwa kujizuia

Mon, 9 Jan 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Yanga wakati wowote kutoka leo itamtambulisha mshambuliaji Kennedy Musona akitokea Power Dynamos ya Zambia, lakini jeuri ya fedha ndefu ndiyo inamshusha Mzambia huyo huku kocha mmoja mkubwa akisema wananchi wamelamba dume haswa.

Taarifa kutoka Zambia ni kwamba Musona ambaye amesajiliwa na Yanga amepewa dili la maana na timu hiyo ya Jangwani na sasa atatakiwa kufanya kazi haswa ili kuwapa imani mashabiki wa timu hiyo.

Dynamos imechukua fedha nzuri katika dili hilo kiasi kisichopungua sh 150 milioni kutoka kwa Yanga ambao wamenunua mkataba wa staa huyo uliokuwa umebaki.

Mbali na klabu hiyo pia Musona mwenyewe amechukua kiasi kama hicho ili kusaini dili la miaka miwili na Yanga huku mshahara wake ukiwa 11 milioni kwa mwezi akiwa kati ya wachezaji wanaolipwa ghali zaidi kwenye Ligi Kuu Bara kwa sasa.

Staa huyo mwenye miaka 29, ambaye anatajwa kuwa alitua nchini jana na kufichwa kwenye hoteli moja ya jiji la Dar es Salaam, akisubiri kutambulishwa na timu hiyo ametoka kwenye timu yake akiwa ndiye kinara wa mabao kwenye Ligi Kuu ya Zambia, baada ya hadi sasa kuwa ameshafunga mabao 11.

Mshambuliaji huyo ambaye aidha watacheza pamoja au mmoja ataanzia nje kati yake na Fiston Mayele mwenye mabao 14 kwenye ligi msimu huu, aliwahi pia kuzichezea Lusaka Dynamos, Zanaco na Green Eagles kwa mafanikio makubwa.

Msikie Lwandamina

Kocha wa zamani wa Yanga na Azam FC George Lwandamina 'Chicken' ameliambia Mwanaspoti kwa simu kuwa Yanga kama wamekamilisha dili la Musona wamepata mtu wa kazi ambaye sio rahisi kuzuiwa na beki mmoja.

Lwandamina alisema Musona ni mshambuliaji mwenye nguvu anayejua kupambana na mabeki wa aina yoyote na kwamba atawasaidia Yanga.

"Nimeona hapa hizo taarifa tangu jana, bila shaka ni usajili mzuri kwa Yanga, huyo ni mshambuliaji mwenye nguvu sio nzuri na rahisi kubaki na beki mmoja kisha akafanikiwa kirahisi kumzuia,"alisema Lwandamina ambaye amelamba dili nono kurejea Zesco ya Zambia.

"Anajua kufunga pia nguvu zake na uwezo wa kumiliki mpira na mbio zake nadhani kwa hapo Tanzania kama akianza vyema tu atafanya vizuri na kuisaidia Yanga."

Chanzo: Mwanaspoti