Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hilika kama Feitoto tu

Hilika 3 Hilika kama Feitoto tu

Sat, 16 Sep 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Moja ya rekodi tamu zilizoandikwa na Wazanzibar msimu huu ni pamoja na wachezaji waliofunga mabao matatu 'Hat trick' za kwanza kwenye Ligi Kuu Bara na Zanzibar kutokea visiwani humo.

Pamoja na ligi hizo mbili kuwa na wachezaji kutoka mataifa mbalimbali, lakini Feisal Salum 'Feitoto' wa Azam FC ndiye nyota wa kwanza kufunga hat trick kwenye Ligi Kuu Bara dhidi ya Kitayosce FC, sawa na Ibrahim Hilika aliyefanya hivyo Ligi Kuu Zanzibar wakati Zimamoto ikiichapa Ngome mabao 5-0.

Feitoto alijiunga na Azam FC msimu huu akitokea Yanga, sawa na Hilka aliyetua Zimamoto akitokepa Polisi Tanzania na wote wameanza kwa moto kwenye ligi wanazoshiriki.

Akizungumza jana, Hilka alisema katika misimu miwili iliyopita hakuwa na wakati mzuri ndani ya Mtibwa Sugar na Polisi Tanzania alizochezea, lakini anaamini msimu huu utakuwa bora kwake akiwa na Zimamoto.

"Mpira ni mchezo wa matokeo, pia morali, kuanza kwa kufunga hat-trick nadhani ni mwanzo mzuri na utaniongezea ari ya kufanya vizuri zaidi.

"Kila mchezaji kuna muda anakuwa kwenye kiwango bora na wakati mwingine anashuka na mimi hali hiyo niliipitia kwenye misimu iliyopita kutokana na sababu mbalimbali, lakini kwa sasa niko fiti na naamini msimu huu utakuwa bora zaidi kwangu," alisema nyota huyo wa Zanzibar Heroes.

Ligi Kuu Tanzania Bara itaendelea leo kwa mechi tatu. KMC itaikaribisha JKT Tanzania, Kitayosce itavaana na Tanzania Prisons na Dodoma Jiji itashuka kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma kucheza na Mtibwa Sugar.

Katika Ligi Kuu Zanzibar zitapiwa mechi mbili leo. Maendeleo FC itakuwa mwenyeji wa KVZ kwenye Uwanja wa Kishindeni na KMKM itakuwa kwenye Uwanja wa Mau A kucheza na Uhamiaji.

Chanzo: Mwanaspoti