Jana jioni uliibuka mjadala kuhusiana na sponsorship baada ya kanuni kuelekeza wachezaji hawaruhusiwi mikataba na kampuni ambazo zinashindana kibiashara na mdhamini wa Ligi Kuu.
Hili ni jambo la kimkataba na yaliyozungumzwa ni utekelezaji wa yaliyomo kwenye mkataba, mkataba uliandaliwa na kusainiwa katika mazingira yapi, ni mkataba unaoeakilisha taasisi zipi, ni mkataba kati ya nani na nani?
Mkataba wa Ligi na TFF kwa niaba ya Bodi ya Ligi ambayo Bodi ndio inasimamia Ligi na TFF inasimama kwa niaba ya Bodi ya Ligi kwenye masuala yote ya mikataba.
Kwa kuwa mkataba unahusu Ligi Kuu moja kwa moja wadau wakubwa wanakuwa ni klabu za Ligi Kuu, kwa hiyo kabla mkataba haujasainiwa na TFF kwa niaba ya Bodi ya Ligi, inabidi klabu zishirikishwe kwa sababu zenyewe ndio zinaenda kutekeleza mkataba huo.
Mkataba unapokwenda hatua ya mwisho ya kusainiwa maana yake wadau wote wanaonufaika na mkataba huo wanakuwa wamehusishwa.
Klabu ndio zinamiliki wachezaji, je ziliangalia hiyo sintofahamu ambayo sasa hivi inajadiliwa kwa maana ya maslahi ya wachezaji?
Tuanzie hapo kwanza kabla hatujajadili mapungufu ambayo yanatajwa na wadau wa michezo.