Mon, 26 Feb 2024
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Simba SC hapaswi kumchukulia poa hata kidogo Jwaneng Galaxy kwani bado anayo nafasi ya kufuzu robo fainali japo ni kwa hesabu ya vidole.
Jwaneng anaweza kufuzu robo fainali endapo atashinda mchezo wake dhidi ya Simba Jumamosi hii Marchi 2, 2024, mchezo utakaopigwa katika Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar.
Akishinda mchezo huo, Jwaneng atakuwa na hesbu za vidole kumuombea ASEC ashinde ugenini dhidi ya Wydad AC na hivyo yeye atakuwa na alama zake 7 zinazomtosha kushika nafasi ya pili chini ya ASEC anayeongoza kundi.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live