Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hiki ndicho kitakachoipa Yanga msimu huu

NABI 2022 Kocha wa Yanga, Mohammed Nasreddine Nabi

Sun, 20 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga, Nesreddine Nabi amefunguka na kusema kuna mambo mawili ambayo yataifanya klabu yake ya Yanga kuibeba Ubingwa wa Ligi Kuu NBC Tanzania kwa msimu huu wa mwaka 2021-2022.

“Yanga wana ukame wa kutwaa taji ndani ya misimu mine, nimefuatilia na nimebaini mapungufu ndani ya misimu hiyo ni ufinyu wa kikosi na kukosa mastaa wenye mwendelezo wa ubora kitu ambacho msimu huu anacho,” alisema Nabi

“Nafurahi msimu huu nimeikuta timu nzuri na ina kikosi kipana ambacho akikosekana mmoja mwingine anachukua nafasi na anafanya kile kinachotakiwa kufanywa,” aliongeza Kocha huyo.

Nabi alisema Yanga ya msimu huu imekuwa na mfululizo wa majeruhi lakini hakuna pengo linaloonekana tofauti na misimu iliyopita na aliongeza kuwa mastaa wake wana ari ya ushindani.

Yanga ndio vinara wa ligi hiyo baada ya kucheza michezo 14 ya mzunguko wa kwanza na kukusanya pointi 36 wakiwa mbele pointi tano na watani zao Simba walio nafasi ya pili na pointi 35.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live