Hiki ndicho kipigo kikubwa zaidi katika historia ya mechi za watani wa jadi (Simba na Yanga) ambapo mchezo huo ulipihwa Julai 19, 1977.
Hapa ndipo ilipozaliwa ‘hat trick’ ya kwanza katika Derby ya Kariakoo iliyofungwa na Abdallah Seif ‘Kibadeni’ King Mputa. Mabao mengine ya Simba yalifungwa na Jumanne Hassan ‘Masumenti’ na jingine la kujifunga la beki wa Yanga, Suleiman Jongo.
Baada ya kipigo hicho Yanga ilijitoa kwenye ligi mwaka 1978 baada ya mechi mbili za awali ambazo zote ilifungwa. Timu hiyo ilijitoa kwa madai kuwa timu yao ilikuwa ikionewa na waamuzi, hivyo kupelekea mwaka huo kutokuwepo mechi kati ya miamba hiyo.
Kufuatia uamuzi huo, mamlaka iliyokuwa ikisimamia mpira wakati huo, Chama cha Soka Tanzania (FAT), kilizipa ushindi wa mabao mawili na alama mbili timu zote zilizotakiwa kucheza na Yanga.