Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hiki ndicho kinachochelewesha kumaliza hadithi ya Harry Kane

Harry Kane Galla Harry Kane

Wed, 19 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ishu ya Harry Kane na Maisha yake pale Tottenham na EPL kwa ujumla na huko nje ya Uingereza ambako vigogo (Real na Bayern) wanamtaka ni mfano wa kitu katika biashara na maisha tunakiita Opportunity Cost.

Opportunity Cost ni faida ambayo ungeweza kuipata kutokana na kile ambacho hukukichagua katika option 2 ulizokuwa nazo. Ni hali ambayo inakulazimu uchague kitu kimoja huku ukiwa tayari kupoteza faida ambazo ungezipata kama ungechagua kingine.

Mfano mwanafunzi ana mtihani kesho na wenzie wamemwalika sherehe usiku wake. Atasoma au ataenda kula good time? Option yoyote itamfanya akose faida ya kile kingine alichokiacha. Ukienda kwa wadau, utakosa muda wa kusoma, ukibaki kusoma jua Cocktail zishakupita.

Harry Edward Kane ndio yupo katika hii situation kwa sasa, (unless akienda United na ambayo nayo inajitafuta kwenye kutwaa mataji makubwa) . Option za kutoka nje ya Uingereza zote zinambana Kane kuchagua moja ya mawili, anataka kuvunja rekodi ya mabao pale England? au uhakika wa mataji (hasa makubwa?).

Abaki England avunje rekodi ya mabao na ayakose mataji makubwa kwengineko au akayafuate mataji makubwa huko uwezekano uliko mkubwa alafu ayasamehe takribani mabao 47 anayotakiwa kufunga ili awe mfungaji bora wa muda wote EPL.

Maamuzi atakayoyachukua yatamgharimu hili ama lile..

Chanzo: www.tanzaniaweb.live