Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hiki ndicho kilichowaua Berkane kwa Mkapa

PAblo MKapa St Pablo Franco Martin

Mon, 14 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya jioni ya jana kuishangaza RS Berkane katika dimba la Mkapa kwa kuichapa goli 1-0.

Kocha Mkuu wa Simba Pablo Franco ameweka wazi kilichowafanya waibuke na ushindi katika mchezo huo wa Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi.

Pablo anasema waliamua kutumia udhaifu wa RS Berkane hasa upande wa kushoto kuanzisha mashambulizi ambayo yaliwafanya kuwa na wakati mgumu muda wote.

"Niliamua kumuanzisha Kibu Denis kwa ajili ya kusaidia kushambulia na kukaba kutokana na uwezo wake licha ya kutoka majeruhi na hakupata muda mrefu wa kucheza.

"Lakini pia udhaifu wao hasa upande wao wa kushoto tuliutumia na tukafanikiwa" amesisitiza Pablo

Chanzo: www.tanzaniaweb.live