Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hiki ndicho kilichopo nyuma ya pazia soka la Cristiano Ronaldo

Skysports Cristiano Ronaldo 5823297 Cristiano Ronaldo

Fri, 11 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Supastaa Cristiano Ronaldo ana balaa kweli kweli. Taarifa mpya zinaeleza kwamba nyota huyo alitaka kuachana na soka kutokana na kubezwa, upweke na maradhi yaliyokuwa yakimsumbua alipokuwa katika kituo cha kukuza vipaji Sporting Lisbon kabla ya kutua Man United.

Kama hujui ni kwamba kabla ya sasa Ronaldo kutambulika miongoni mwa wachezaji bora duniani kutokana na kuutendea haki mchezo wa soka, staa huyo alivumilia mambo mengi ambayo alipitia akiwa na miaka 12.

Inadaiwa kwamba alikuwa akipata wakati mgumu kufiti na watoto wenzake jijini Medeira, Ureno katika masuala ya soka, lakini nyota huyo akatoboa katikati ya tabu zote alizopitia utotoni.

Sporting Lisbon ilimsajili Ronaldo akiwa na miaka 12 kwa mujibu wa kitabu kimoja kutoka Ureno kilichoandika historia yake.

Kitabu hicho kinaeleza alitaka kuondoka Sporting Lisbon kabla ya kupandishwa kikosi cha wakubwa, huku bosi wa klabu hiyo akitishia kumtimua na kumrudisha nyumbani.

Ronaldo alilazimika kuachana na masuala ya shule ajikite katika soka zaidi kwani ni mchezo aliokuwa akiupenda kuliko kitu chochote.Ikumbuke kwamba aliwahi kuweka wazi kuwa elimu ni kitu ambacho alikuwa hakipendi tofauti na soka.

Staa huyo alipofika miaka 14, alijipanga upya kwa tizi za kuujenga mwili kwani kipindi hicho alikuwa mwembamba sana licha ya kupigwa biti na viongozi wa Sporting kila mara kutokana na sababu mbalimbali.

Mafanikio ya Ronaldo yalianza kuonekana alipojiunga na Man United 2003 kabla ya kwenda Real Madrid 2009 na baadaye akatimkia Juventus 2018 ilhali sasa amerejea Old Trafford baada ya miaka 12. Kwa sasa staa huyo anapitia kipindi kigumu baada ya kuanza msimu kwa kusuasua.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live