Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hiki ndicho kilichomkimbiza Bangala Yanga

Bangalaa.jpeg Yannick Bangala

Wed, 26 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maneno bado ni mengi, maswali yasiyokuwa na majibu yanazuka kila kukicha huku wenye majibu ya maswali hayo wakiwa wako kimya pasina kutoa majibu juu ya sababu za kuondoka kwa Kiungo Yannick Bangala katika Klabu ya Yanga,

Sasa hebu tuchambue kwa kiwango cha Uwanjani pengine tunaweza kupata sababu hasa za Bangala kutokuwa katika Kikosi cha Yanga

Nabi alihitaji Nidhamu na kujituma Zaidi.

Wakati Kocha Nabi akibadilisha Mfumo kutokana na Wachezaji anao amini kwake wana nidhamu kubwa ya Nhe ya Uwanja na Kiuchezaji, Ilimlazimu kubadili mfumo kutoka 4-3-3 hadi kuwa 3-4-3,

Mfumo wa 4-3-3 Ulimbeba zaidi Bangala kwenye eneo la kiungo kabla ya Nabi kuamua kumuweka benchi na kuja na Mfumo wa 3-4-3 ambao ulifanya aanze na walinzi wa 3 ambao ji Bacca,job na Mwamnyeto,

Bangala aliomba kuondoka Yanga

Uongozi wa klabu ya Yanga haukuwa tayari kuachana na Kiungo wao Yannick Bangala ila Yeye Bangala ndio aliomba kuondoka Yanga Sc huku ikifahamika kuwa alishaingia kwenye mazungumzo na klab ya Azam ambayo ilikuwa tayari kumuacha Issah Ndala ili aingie Bangala,

Maneno ya Bangala yalizidi kukiotesha kibarua chake Nyasi kwakuwa Uongozi na Benchi la Ufundi ulichukizwa zaidi kwa Mchezaji ambaye bado Mkataba nao,

Alisema Yannick Bangala

"Nina asilimia 20% pekee za kusalia Yanga Sc kwa msimu ujao huku asilimia 80% za kuondoka ”.

Uongozi wa Yanga Haukuridhiswa wa kufurahishwa na Maneno hayo na ndipo ulipoanza haraka kutafuta mbadala wake kwakuwa walishajua hatokuwa tena sehemu ya kikosi chao kutokana na sababu mbali mbali.

Mpaka sasa Uongozi wa Yanga haupo tayari kuendelea nae kwani unaamini Yannick sio Mwalimu Mwema ndani ya Yanga kwa vijana na badala yake Juma hili watakaa tena kujua nini kifanyike licha ya Bangala kugoma kwenda Singida Fg kwa Mkopo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: