Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hiki ndicho kilichoipa Man United Ubingwa wa UEFA 2008

Fergie Evra Hiki ndicho kilichoipa Man United Ubingwa wa UEFA 2008

Tue, 17 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mlinzi wa zamani wa Man United Patrice Evra ameainisha kitu kilichowasukuma kuwapa ushindi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2008 dhidi ya Chelsea.

Katika mchezo huo wa Fainali uliopigwa Moscow ulimalizika kwa sare ya bao 1-1 lakini United walishinda kwa mikaju ya penati 6-5.

Akizungumza Evra anasema;

"Ferguson alisema: 'Tayari nimeshinda. Hatuhitaji hata kucheza mchezo huu.' Tukawa tunashangaa, Anazungumza nini huyu? Mechi hata haijaanza.

Kisha Ferguson akanigeukia, akawaambia 'Mtazameni Patrice,' akasema. 'Evra Ana kaka na dada zake wengi. Hebu wazia kile ambacho mama yake alilazimika kufanya ili kuweka chakula mezani!'

Kisha akamgeukia Wayne Rooney: 'Mtazame Wayne. Alikulia katika moja ya sehemu ngumu zaidi ya Liverpool.' Kisha akamgeukia Park Ji-sung; 'Angalia Ji, amekuja kutoka Korea Kusini.'

Wakati bosi anazungumza kuhusu hadithi zetu, tulianza kutambua kwamba alikuwa akimaanisha tushirikiane. Hatukuwa timu ya soka tu bali tulikuwa ni watu kutoka kila kona ya dunia, kutoka kila aina ya tamaduni, rangi na dini tofauti.

Lakini tupo pamoja katika chumba kimoja cha kubadilishia nguo ndani ya Moscow, tukipambana Kupitia mpira wa miguu, sisi ni ndugu.

Ferguson akasema 'HUU ndio ushindi wangu' Baada ya Maneno yake wote tulipata goosebumps. Kisha tukacheza na kushinda Ligi ya Mabingwa. Hiyo ndiyo Manchester United. Ndio maana siku zote nasema "I love this Game"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live