Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hiki ndicho kikosi bora cha Mesut Ozil

Mesu Ozil Mesut Ozil

Fri, 24 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mesut Ozil ametaja kikosi chake bora cha wachezaji ambao alicheza nao Arsenal, Alexis Sanchez na Santi Cazorla wakiwemo kwenye kikosi hicho.

Hiyo ni baada ya kutangaza amestaafu kucheza soka akiwa na umri wa miaka 34, lakini kiungo huyo aliyekuwa akikikpiga Istanbul Basaksehir kutoka Uturuki amesema, kipindi anaichezea Arsenal alizungukwa na wachezaji hatari wenye viwango bora.

Aidha Ozil Alishukuru klabu zote alizowahi kuzichezea, Real Madrid, Werder Bremen, Fenerbahce na Schalke O4, akikiri majeraha ya mara kwa mara yamesababisha astaafu kucheza soka mapema, lakini ataendelea kukumbuka mafanikio aliyopata katika maisha yake ya soka.

Kiungo huyo aliulizwa swali wachezaji gani bora ambao aliwahi kucheza nao wakati anakipiga Arsenal, Ozil akajibu kwa kuanzia safu ya mabeki na kipa "David Ospina, Bacary Sagna, Laurent Koscielny, Per Mertesacker na Sead Kolasinac". Kwenye safu ya kiungo Ozil akawataja Aaron Ramsey, Santi Carzola.

Baadaye Ozil akajitaja kwenye kikosi hicho kama kiungo anayecheza namba 10, sambamba na Serge Gnabry ambaye alicheza winga anayetokea kulia, upande wa kushoto akamtaja Sanchez. Kwenye safu ya ushambuliaji Ozil akamtaja Pierre-Emerick Aubameyang ambaye sasa anakipiga Chelsea.

Ozil aliipotezea Tottenham baada ya kuulizwa swali je angekuwa tayari kujiunga na timu hiyo endapo angepewa ofa na timu hiyo kiungo huyo akajibu "Swali rahisi nastaafu kucheza soka".

Ozil soka lake lilianza kujulikana kipindi anakipiga Schalke mwaka 2006 kabla ya kujiunga na Werder Bremen mwaka 2008, Kutokana na kiwango chake bora alichoonyesha Bundeliga, Ozil akasajiliwa na Madrid kwa kitita cha Pauni 13 milioni. Ozil akabeba mataji mbalimbali Santiago Bernabeu kama Copa del Rey na La Liga kabla ya kujiunga na Arsenal.

Arsenal ilivunja rekodi ya usajili ilipomsajili Ozil kwa kitita cha Pauni 42.5 milioni mwaka 2013 kiungo huyo akawa shujaa wa klabu ndani ya viunga vya Emirates. Alifunga mabao 44 katika mechi 254 alizocheza akiisaidia Arsenal kubeba mataji matatu ya Kombela FA ndani miaka minne baadaye akafanikiwa kubeba ubingwa wa Kombe la Dunia akiwa na kikosi cha Ujerumani mwaka 2014.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live