Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hiki ndicho Chanzo cha Shaffih Dauda kufungiwa, awaita TFF Madikteta (+Video)

DAUDA Mchambuzi wa Soka, Shaffih Dauda

Thu, 17 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jumatano ya Februari 16, Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TTF, ilitoa adhabu ya Kumfungia kujihusisha na Soka ndani na nje ya nchi kwa muda wa Miaka mitano Sambamba na kulipa faini ya Shilingi milioni 6.

Sasa Shaffih mwenyewe amefunguka sababu hasa zilizopelekea kukumbana na kadhia hiyo, huku akiweka wazi hisia zake na namna alivyo huru kuzungumzia soka baada ya adhabu hiyo.

Mbali na hilo Shaffih pia amefafanua maeneo ambayo anazuiwa na adhabu hiyo tofauti na wengi walivyodhani.

Soma hapa chini andiko ambalo limesababisha Mchambuzi huyo kuitwa mbele ya Kamati ya Maadili ambalo lilichapishwa katika ukurasa wake wa Instagram Februari 8 mwaka huu.

"TFF NI NYUMBA YA KUPANGA?"

TFF ni taasisi yenye kusimamia maslahi ya mpira wetu, TFF sio nyumba ya kupanga ambayo Baba mwenye nyumba aseme hiki tufanye hiki tusifanye hata kama hakina maana

TFF sio nyumba ya kupanga ambayo Mwenye nyumba aseme leo nyama hapana, aseme sitaki Mtu abandike picha ukutani na kuhojiwa kusiwepo! TFF ni mali yetu wote

Shida kubwa iliyopo Shirikisho ni mentality ya nyumba ya kupanga, wakisema kitu sisi Wapangaji tusihoji kwakuwa hatukuchangia tofari wala madirisha, wala hatukutoa mia ya uwanja, SIO KWELI

Wakati mmesaini mikataba yote klabu hawajui kitu zaidi ya kupelekewa figure na kuambiwa watekeleze, hakuna kuhoji bali kutekeleza, huo sio uongozi bali DICTATORSHIP

Klabu zimeenda kutekeleza kitu ambacho hawajui msingi wake, ndani ya miaka miwili wadhamini wawili wanaondoka bila fidia kwa klabu, shida kubwa ikiwa ni ninyi TFF na Mentality za BABA MWENYE NYUMBA

TPLB ipo kwa ajili ya maslahi ya klabu zote ila mmeitoa meno, mmeifanya kama kamati na ninyi mmejipa majukumu yote, TPLB haina Viongozi bali CEREMONIAL LEADERS, Kila kitu kinafanyika Karume

Matokeo yake ndio haya! Mguto hana makosa, Kasongo hana makosa tena wasipewe jumba bovu tatizo lote ni ninyi hapo KARUME, ndio maana siku zote huwa nawaambia bodi iwe huru isajiliwe kama Kampuni

Kila siku agenda lakini mpo kwenye total failure! Nyie msimamie mpira, nyie msimamie timu za taifa, nyie msimamie Ligi, Guys muelewe DIVISION OF POWER haikwepeki, mjitathimini ikiwemo hata kujiuzulu sio kwa ubaya

Kila mkataba kisheria ambao TPLB atasaini ninyi mnapata 10% kisheria, tatizo nini mtake kila kitu mfanye ninyi??? Kuna siri gani ambayo hatuijui

Whenever we are given an oppurtunity to elect leaders, we are given a blank cheque! We elect hyenas to take care of goats

When DIGALA speaks????_______"

Sasa Andiko hili lilisababisha akaitwa mbele ya Kamati ya Maadili na vikao vya Kamati hiyo vikampa adhabu husika.

Msikilize Shaffih akifafanua kwa undani;

View this post on Instagram

A post shared by Valor (@valorsportstz)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live