Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hiki hapa kikosi cha Chelsea 2030

Chelsea Pict Hiki hapa kikosi cha Chelsea 2030

Wed, 4 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Straika, Nicolas Jackson ameingia kwenye orodha ya mastaa waliosaini mikataba mirefu huko Chelsea.

Straika huyo mkataba wake mpya huko Stamford Bridge aliosaini hivi karibuni utafika ukomo 2033, akiwa mchezaji mwingine wa miamba hiyo ya The Blue aliyesaini dili refu.

Chelsea sasa ina wachezaji 20 wenye mikataba itakayowafikisha muongo mwingine wakifanya hivyo ili kukwepa adhabu ya kukiuka kanuni za matumizi na mapato za Ligi Kuu England.

Kwenye dirisha la usajili lililofungwa hivi Ijumaa iliyopita, Chelsea ilisajili makipa wawili. Mike Penders, 19, kutoka Genk kwa Pauni 17 milioni na Filip Jorgensen, 22, kutoka Villarreal kwa Pauni 20.7 milioni na winga Jadon Sancho kutoka Manchester United kwa mkopo.

Jorgensen na Penders wamesainishwa mikataba mirefu itakayovuka muongo huu, hivyo wanaweza kuwa sehemu ya kikosi cha Chelsea mwaka 2030.

Renato Veiga, atakuwa beki wa kushoto, beki wa kati au kiungo baada ya kusaini miaka saba akitokea Basel, beki wa kulia ni Malo Gusto, wakati beki wa kati ni Aaron Anselmino, atacheza pacha na Benoit Badiashile, 23, mwenye mkataba hadi 2030.

Kwenye kiungo kutakuwa na wakali wawili ambao Chelsea ilivunja rekodi ya uhamisho kuwasajili, Enzo Fernandez na Moises Caicedo, waliogharimu zaidi ya Pauni 200 milioni.

Fernandez, 23, mkataba wake hadi 2032, wakati Caicedo, 22, yupo Stamford Bridge hadi 2031 na kuna kipengele cha kuongeza mwaka. Kwenye fowadi kuna Cole Palmer, 22, mwenye mkataba hadi 2033, Estevao Willian, 17, mwenye mkataba hadi 2033, Kendry Paez na Jackson.

Mastaa wengine wenye mikataba mirefu ni Mykhailo Mudryk, 23, Joao Felix, 24, na Pedro Neto, 24, ambao dili zao zitafika tamati 2031, huku Noni Madueke, 22, na mkali mpya Kiernan Dewsbury-Hall, 25, mikataba yao itafika mwisho 2030.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live