Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hijjah Shamte, kinda mpambanaji

Hijjah Shamte Hijjah Shamte, kinda mpambanaji

Sun, 17 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hijjah Shamte, kiungo mkabaji wa timu ya Kagera sugar na timu ya taifa ya Tanzania under 18 na under 20, ni moja kati kipaji kilichoibuliwa na kocha Meck mexime wakati akiwa Cambiaso Academy.

Ni mchezaji mwenye umri mdogo ila anavutia akicheza uwanjani, anakaba vizuri na anauwezo mkubwa wa kuichezesha timu kutoka nyuma.

Shamte ni kati ya wachezaji waliong'ara sana kwenye michuano ya cecafa under 18 yaliyomalizika nchini kenya mapema mwezi huu.

Pia, ni moja ya wachezaji wenye uwakika wa kuanza kwenye kikosi cha kwanza cha Kagera sugar licha ya umri mdogo alionao.

Naamini msimu huu atakuwa ni kati ya wachezaji watakaowania tuzo ya mchezaji bora chipukizi wa NBC premier league.

Kama ataendelea kupambana namwona akifika mbali kwa siku za mbeleni na hata akiwa miongoni mwa wachezaji muhimu wa Tanzania kwenye Afcon 2027 itakayofanyika Katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live