Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hii ya kufurahia mwenzako kutolewa badala ya kuumia wewe kutolewa imekaaje?

Ahmed Kamwez Kamwe na Ahmed.

Tue, 9 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wacha turudi upande wa Meneja habari na mawasiliano Yanga SC, Ali Shaban Kamwe baada ya na yeye kurudi salama nyumbani akitokea nchini Afrika Kusini ambapo Kikosi cha Yanga kilikuwa na kibarua kizito mbele ya Mamelodi Sundowns.

Mchezo ule ulimalizika kwa Yanga SC kukubali kupoteza mchezo kwa changamoto za mikwaju ya PENATI mbele ya huyo mpinzani wake Mamelodi. Lakini mambo kadhaa yalijitokeza likiwemo lile tukio SUGU la MWAMUZI kushindwa kutafsiri tukio la mpira kuingia golini mpira uliopigwa na kiungo Stephanie Aziz Ki.

Matokoe yale yalibua Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano Simba SC, Ahmed Ally na kuonyesha kufurahishwa zaidi na kusema, amefurahi na kutaka watani zake YANGA SC waone na wajifunze katika hilo.

Kwa upande wa Ali Kamwe ameonyesha kushangwaza kwa tukio hilo la Ahmed Ally na kusema ni kama rafiki yake huyo ameanza kupoteza kitu kwenye majukumu yake ya kazi, akaongeza utautafuta muda mzuri ili aweze kushauri ili aachane na mambo kama hayo.

Eti wakati mwingine Yanga SC ikishinda mechi Ahmed Ally anaweza kwenda chooni na kushangilia bao kwani ni wazi hua anayo mapenzi Kwa Yanga SC kama ilivyo kwa watu wengine, na zaidi siyo kama Ahmed Ally amefurahi Yanga SC kutolewa lakini pia amefurahia zaidi Simba SC kuendelea kukwama kusonga mbele hatua ya Nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa.

Je ni kweli wadau wengi wa Soka nchini wengi ni mashabiki wa Yanga SC?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live