Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hii timu ya Zidane, kila kombe inachukua!

Dsvds Zidane Hii timu ya Zidane, kila kombe inachukua!

Tue, 2 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwaka 2014, gwiji wa Real Madrid, Zinedine Zidane alitaja Kikosi cha Kwanza cha wanasoka bora kabisa duniani.

Alifanya hivyo katikati ya msimu 2014-15 wakati huo akiwa kwenye kikosi cha Real Madrid B, kabla hata hajapata nafasi ya kukinoa kikosi cha kwanza cha Los Blancos, Januari 2016.

Kwenye kikosi chake cha Zidane, kulikuwa na mastaa wengi sana wa Real Madrid nap engine hilo lilimvutia rais wa Los Blancos, Florentino Perez kumpa jukumu la kunoa kikosi cha kwanza cha miamba hiyo ya Santiago Bernabeu.

Fundi huyo wa mpira wa zamani wa timu taifa ya Ufaransa, timu yake ilihusisha pia mastaa wa Barcelona, hivyo jambo hilo linaonyesha kwamba aliweka pembeni ushabiki na utimu kwa kuchagua wachezaji wa timu ya pinzani.

Na sasa ikiwa karibu miaka 10 imepita, tunajaribu kuwaangazia mahali walipo mastaa hao waliotajwa na Zidane kwenye Kikosi cha Kwanza, wako wapi.

Kwenye benchi lake, mastaa waliotajwa na Zidane ni Manuel Neuer, Phillip Lahm, Raphael Varane, Franck Ribery, Paul Pogba, Andres Iniesta na Sergio Aguero.

Kipa: Iker Casillas

Moja ya zao bora kabisa kutoka kwenye akademia ya La Fabrica. Kipa Casillas alishinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya na klabu yake ya Real Madrid siku nne tu baada ya kutimiza umri wa miaka 19. Baadaye, kipa Casillas akiwa mdogo, alipoteza nafasi kwa kipa Cesar Sanchez katika fainali ya 2002, wakati Zizou alifunga bao matata kabisa dhidi ya Bayer Leverkusen, lakini aliingia kutokea benchini na kuokoa hatari nyingi kuifanya Madrid kulinda goli lao.

Alibaki kuwa kipa imara wa Real Madrid hadi iliponyakua taji La Decima mwaka 2014, ambapo Zidane alikuwa kocha msaidizi wa Carlo Ancelotti. Aliondoka na kwenda kujiunga na Porto miezi sita kabla ya Zidane kurithi mikoba ya Rafael Benitez kwenye kikosi cha kwanza huko Bernabeu.

Alistaafu soka 2020 baada ya miaka mitano huko Porto, ambapo alipata tatizo la maradhi ya moyo. Tangu wakati huo yupo tu nyumbani.

Beki wa kulia: Dani Alves

Chochote alichofanya Alves ndani ya uwanja kwa sasa hakipewi sita kubwa sana kutokana na namna maisha yake ya soka yalivyomalizika. Mbrazili huyo alikutwa na hatia ya kumbaka mwanamke kwenye klabu moja ya starehe za usiku, Desemba 2022 na kuhukumiwa kifungo cha miaka minne na nusu jela. Ametoka kwenye gereza la huko Barcelona baada ya kulipa dhamana ya Euro 1 bilioni.

Beki wa kati: Pepe

Beki matata kabisa wa Kireno aliyetamba kwa zaidi ya muongo mmoja kwenye kikosi cha Real Madrid na kuachana na timu hiyo mwaka 2017 baada ya kushinda mataji matatu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Zidane wakati alipokuwa kocha kwenye kikosi hicho, alimtupa benchi Pepe na kumpa nafasi Mfaransa mwenzake, Raphael Varane.

Baada ya miezi 18 akiwa na Besiktas, alikwenda kujiunga na Porto kama mchezaji huru Januari 2019. Bado anakipiga kweye kikosi hicho kwa miaka mitano sasa, akicheza zaidi ya mechi 200 kwenye kikosi hicho chenye maskani Estadio do Dragao. Yupo kwenye kikosi cha Ureno kilichopo kwenye fainali za Euro 2024, akiwa mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi katika fainali hizo za Ujerumani. Akiwa na miaka 41.

Beki wa kati: Sergio Ramos

Baada ya kuondoka Casillas mwaka 2015, Ramos – ambaye alicheza na Zidane kwenye mechi yake ya kwanza alipotua Bernabeu – alifanywa kuwa nahodha wa klabu hiyo, ambapo alikuwa kiongozi wa uwanjani wa kikosi cha Zizou. Wakati huo, tayari Ramos alikuwa amecheza mechi yake ya 450 kwenye La Liga, Julai 2020, alipochaguliwa kuwa nahodha wa huko Bernabeu.

Tangu alipoondoka Madrid mwaka 2021, Ramos alikwenda PSG, alikocheza kwa miaka miwili sambamba na Lionel Messi kabla ya kurejea kwenye klabu yake ya utotoni ya Sevilla. Ameachana na timu hiyo kwa mara ya pili, lakini bado hajatangaza atakwenda wapi, huku Ligi Kuu Marekani na Saudi Pro League zikitajwa kuwa na mpango wa kumnasa kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi.

Beki ya kushoto: Marcelo

Baada ya miaka 15 na kucheza zaidi ya mechi 500, Marcelo aliachana na Madrid baada ya kushinda taji la tano la Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2022. Alikuwa nahodha wa timu hiyo, kabla ya kujikuta kwenye wakati mgumu alipokuwa akisugua benchi kwenye miaka yake mwishoni katika timu hiyo.

Alitimka kwenye kujiunga na Olympiacos kwa uhamisho huru, lakini hakudumu sana huko Ugiriki, aliondoka na kurudi kwao Brazil kwenda kujiunga na Fluminense, ambayo ilimsaidia kuongeza taji jingine kwenye kabati lake, baada ya kunyakua Copa Libertadores mwaka jana.

Kiungo wa kati: Yaya Toure

Baada ya kupata mafanikio makubwa akicheza na Claude Makelele kwenye klabu na timu ya taifa, ilidhaniwa kwamba Zidane angemchagua mchezaji huyo kwenye kiungo ya kukaba, kama ambavyo alipata huduma bora kutoka kwa Casemiro kwenye kipindi chake cha ukocha. Lakini, Zizou alikuwa na chaguo jingine kabisa na kumtaja Yaya Toure, aliyekuwa moto kwenye kikosi cha Barcelona chini ya kocha Pep Guardiola. Baadaye, Toure alitimkia zake Manchester City alipokwenda kuwa moto uwanjani.

Aliachana na Man City mwaka 2018 na kutimkia Olympiacos, ambako pia hakudumu sana kama Marcelo na hivyo kwenda zake China kujiunga na timu ya Qingdao Huanghai. Baadaye alienda kuwa kocha wa akademia za Olimpik Donetsk, Akhmat Grozny, Tottenham, Standard Liege kabla ya sasa kumsaidia Roberto Mancini huko Saudi Arabia.

Kiungo wa kati: Luka Modric

Jina lililoshtua kwenye kikosi hicho cha kocha Zidane, licha ya kwamba kipaji cha mchezaji huyo kinaondoa maswali yote kwanini amepata nafasi kwenye timu hiyo ya gwiji huyo wa Ufaransa, ambapo staa huyo wa Croatia alisimama vyema kwenye kiungo wakati Madrid inabeba La Decima msimu wa 2013-14.

Tangu wakati huo, Modric ameshinda mataji mengine matano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Real Madrid, ambako ataendelea kucheza kwa msimu moja zaidi. Mwaka 2018 alishinda Ballon d’Or baada ya kuisaidia Croatia kufanya vizuri kwenye fainali za Kombe la Dunia huko Russia, ambapo timu ilifika fainali.

Winga wa kulia: Zlatan Ibrahimovic

Kwenye upande wa kulia katika kikosi cha kwanza cha Zidane, mchezaji aliyepeta nafasi ni Zlatan Ibrahimovic. Staa huyo alikuwa kwenye kiwango bora kabisa kwenye kikosi cha PSG, huku akipita pia kwenye timu za Juventus, Inter Milan, AC Milan, Barcelona na Manchester United, ukiachana na Malmo na Ajax alizochezea utotoni.

Baada ya kuzurura kwenye timu nyingi za Ulaya na kisha kwenye Marekani, Ibrahimovic alitangaza kustaafu soka kwenye kipindi cha majira ya kiangazi yam waka jana wakati alipokuwa kwenye kikosi cha AC Milan, ambako alicheza mechi nne tu kutokana na kuwa majeruhi. Kwa sasa ni mshauri mkuu wa kikosi cha Rossoneri.

Kiungo mshambuliaji: Lionel Messi

Zidane aliwahi kumsifu Lionel Messi kwamba amekuwa akiona vitu uwanjani kabla ya mtu mwingine kuviona. Zidane anafahamu wazi Messi alikuwa kwenye kikosi cha wapinzani wa timu yake ya Real Madrid, lakini hilo halikumfanya kubisha juu ya uwezo wa Muargentina huyo, ambaye baada ya kuachana na Barcelona, alikwenda Barcelona na kisha kuhamia zake Inter Miami ya Marekani.

Messi aliisaidia Argentina kushinda ubingwa wa Kombe la Dunia 2022 katika fainali zilizofanyika Qatar na sasa anakitumikia kikosi hicho katika mikikimikiki ya Copa America 2024 huko Marekani.

Winga wa kushoto: Cristiano Ronaldo

Ronaldo alifunga mabao 112 katika mechi 114 alizocheza chini ya Ancelotti, huku nyakati bora zaidi alizowahi kupata kwenye kikosi cha Real Madrid ni wakati alipokuwa kikosi cha Jose Mourinho.

Ronaldo, ndiye kinara wa mabao wa muda wote wa Los Blancos na alikuwamo kwenye kikosi cha Bernabeu kilichobeba mataji matatu mfululizo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya chini ya Zizou. Aliondoka kwenye Juventus, kisha Manchester United kabla ya kutimkia Saudi Arabia kujiunga na Al Nassr. Kwa sasa Ronaldo yupo kwenye kikosi cha Ureno kinachocheza fainali za Euro 2024, akicheza mikikimikiki hiyo ya kusaka ubingwa wa Ulaya huko Ujerumani akiwa na umri wa miaka 39.

Straika: Karim Benzema

Katika kukamilisha kikosi chake cha kwanza, Zidane alimchagua mchezaji wa saba kwenye kikosi cha Real Madrid na kumpa nafasi katika kikosi chake.

Hakuna mchezaji aliyecheza mechi nyingi kumzidi Benzema katika kikosi cha Real Madrid ya Zidane. Staa huyo alionyesha kiwango bora kabisa baada ya kuondoka Ronaldo na kufanikiwa kushinda Ballon d’Or baada ya kufanya vizuri katika kikosi cha Real Madrid na timu ya Ufaransa. Aliondoka Real Madrid mwaka jana kwenda kujiunga huko Saudi Pro League kwenye kikosi cha mabingwa Al-Ittihad, ambako pia mambo hayakwenda vizuri baada ya kuumia kwenye msimu wake wa kwanza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live