Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hii ni vita ya ubabe Championship

Pamba Jiji FC CHAM Pamba Jiji FC

Wed, 3 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Championship ikibakiza mechi tatu kumaliziaka huku presha ikiendelea kuwa ngumu katika nafasi mbili za juu, huenda vita ya mabao ikaamua hatima ya timu za kupanda Ligi Kuu msimu ujao.

Hadi sasa timu zote zimecheza mechi 27 zikibakiza tatu, huku Ken Gold wakiwa kileleni kwa pointi 61, Pamba Jiji wakifuata  alama 58, Biashara United wamevuna 56 sawa na Mbeya Kwanza, ilhali TMA wakiwa na alama 54 katika nafasi ya tano.

Katika mechi zinazofuata, TMA itakuwa nyumbani kuwakaribisha Ken Gold,  hukuwa Pamba Jiji wakiwa wageni wa Mbuni, Mbeya Kwanza wakiwaalika Transist Camp na Biashara United wakiwapokea Green Warriors mjini Musoma mkoani Mara.

Katika matokeo ya mechi za wikiendi yalionekana kuamsha upya vita ya kupanda daraja kwa timu mbili za juu, haswa ishu ya mabao ikionekana kushika kasi kwa kila upande katika zile za nafasi tatu za juu.

Katika mechi hizo, Ken Gold walilazimishwa sare ya 3-3 mbele ya Mbuni, Pamba Jiji ikainyoosha Polisi Tanzania 5-1 sawa na Biashara United iliyoikanda Transit Camp,  Mbeya Kwanza nao wakashinda 1-0 dhidi ya FGA Talents na TMA ikailaza Mbeya City 2-1.

Hadi sasa Biashara United ndio inaongoza kwa idadi kubwa ya mabao ya kufunga (52) ikiruhusu 19, Pama Jiji ikifunga 48 na kuruhusu 16, Ken Gold imefunga 47 na kufungwa 18, Mbeya Kwanza ikiingia wavuni mara 44 na kuruhusu 26 huku TMA wakifunga 37 na kuungwa 18.

Hata hivyo, iwapo kila timu itashinda mechi zote Ken Gold itafikisha alama 70, Pamba Jiji 67, Biashara United pointi 65 sawa na Mbeya Kwanza huku TMA ikiishia 61 japo katika michezo hiyo baadhi wapinzani watakutana na kusababisha kupungua kwa pointi.

Hesabu za Biashara United na Mbeya Kwanza ni kumuombea Pamba Jiji katika michezo yake miwili ya mwisho ugenini dhidi ya Mbuni na TMA zinaiombea dua mbaya ili ipoteze ili kubaki na pointi 61 za uhakika kwa timu hizo ziweze kuamuliwa kwa mabao.

"Kila mmoja ashinde mechi zake. Sisi tunaendelea kupambana, tunapofanikiwa kumzidi mpinzani akaingia kwenye mfumo ni kumfunga idadi kubwa ya mabao kama tulivyofanya huko nyuma" amesema kocha mkuu wa Biashara United, Aman Josiah.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live