Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hii ndiyo sababu ya picha ya Ronaldo kuondolewa Olf Trafford

Ronaldo Msk.jpeg Hii ndiyo sababu ya picha ya Ronaldo kuondolewa Olf Trafford

Thu, 17 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maafisa wa uwanja wa Old Trafford wameanza kuondoa mabango yenye picha za nyota wa klabu hiyo na timu ya Taifa ya Ureno, Christiano Ronaldo.

Picha mbalimbali zimewaonesha maafisa wa uwanja huo wakibandua picha hizo ambazo zimewekwa kuzunguka uwanja wa Old Trafford.

Mapema wiki hii jina la Ronaldo liligonga vichwa vya habari katika maeneo mbalimbali duniani baada ya nyota huyo wa soka kueleza mambo kadhaa yanayozunguka klabu ya Manchester United katika mahojiano ya “Talk Tv” yaliyoendeshwa na Piers Morgan.

Wengi wanaamini kuwa picha ya Ronaldo ambayo yupo na Beckam pmaoja na Cantona kwa ajili ya promo ya jezi namba 7 imeondolewa kwa sabbau ya mahojiano yake ambayo alisema hamuheshimu kocha wa Manchester United kwa sabbau yeye pia hamuheshimu.



kupitia mitandao mbalimbali watu wengi wamesema kuwa United inaodoa hilo bango kwa sabbau ya kuwekwa mabango mengine maana Uwanja wa Old Trafford utatumika kwenye fainali ya mchezo wa Rugby Novemba 19.

Hata hivyo website ya Manchester United imethibitisha kuwa taraehe 19 ambayo ni Jumamosi itafanyika fainali ya mchezo wa Rugby.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live