Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hii ndio siri ya ushangiliaji kwa Angel Di Maria

Angel Di Maria Argentina Final World Cup Mundial 2022 121822 (1) Hii ndio siri ya ushangiliaji kwa Angel Di Maria

Wed, 18 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wachezaji wengi wamekuwa na utaratibu wa kushangilia kwa style tofauti tofauti wanapofunga goli na kila mchezaji anakuwa na sababu ya kushangilia kwa style hiyo.

Angel Di Maria mchezaji wa timu ya Taifa Argentina na klabu ya Benfica ambaye anaweza kucheza kama winga au kiungo mshambuliaji ana style yake ya ushangiliaji ambayo kila anapofunga goli amekuwa akishangilia, nyota huyo amefunguka kwenye moja ya mahojiano na kusema kwanini amekuwa akiweka ishara ya moyo anaposhangilia akimaanisha upendo.

Di Maria anasema wakati anatoka Argentina sehemu ambayo alizaliwa na kwenda kuanza maisha kama mchezaji wa kulipwa kule Ureno kwenye klabu ya Benfica, kabla hajaondoka alimbembeleza mchumba wake wa muda wote kwenda nae Ureno lakini mrembo huyo Jorgelina Cardoso aligoma kabisa kusafiri na mwana kwenda kutafuta maisha Ureno.

Baada ya muda kupita Di Maria akiwa Ureno na mlimbwende huyo akiwa Argentina bibie alikubali kukwea pipa na kumfata mwana Ureno ili waishi wote kama ambavyo Di Maria alikuwa anatamani iwe.

Sasa siku ambayo Jorgelina Cardoso mchumba wa Di Maria alitua Ureno, Benfica walikuwa uwanjani wakicheza mechi ya ligi na Di Maria aliweka wavuni goli moja, wakati huo mrembo alikuwa jukwaani akimwangalia Di Maria hapo ndo Di Maria alipoenda kwenye lile jukwaa kushangilia kwa kuonyesha ishara ya moyo wa upendo, hii ilikuwa na maana kuwa bibie ameonyesha upendo mkubwa kutoka Argentina na kutua Ureno kuishi na mwana ambaye anajitafuta kwenye career ya mpira.

Upendo umekuwa na nguvu kwa na umeamua vitu vingi sana kwenye haya maisha Badae Di maria alihama Benfica na kujiunga na Real Madrid, Manchester United, Paris Saint Germain, Juventus na sasa amerudi tena Benfica lakini ikumbukwe mwaka 2011 walifunga ndoa wapendanao hao na hadi leo bado style yake ya kushangilia haijawahi kubadilika.

Mapenzi yana nguvu kwenye huu ulimwengu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live