Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hii ndio sifa ya ziada ya Jobe Simba SC

Hii Ndio Sifa Ya Ziada Ya Jobe Simba SC.jpeg Hii ndio sifa ya ziada ya Jobe Simba SC

Tue, 5 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Pa Omar Jobe ni ingizo jipya ndani ya Wekundu wa Msimbazi Simba SC, na tayari ameshaonesha cheche zake kwa kufunga magoli ikiwemo mechi ya mwisho ya Hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy.

Mchambuzi wa soka Bongo, George Ambangile amesema moja kati ya sifa kubwa aliyonayo Jobe ni kitendo cha kuwa na uwezo wa kutotulaia sehemu moja pindi anapokuwa uwanjani.

"Anaweza kushuka chini, anaweza kuutanua uwanja na ndio maana unaona iliwapa nafasi sana viungo wa Simba kina Chama na wenzake kufanya vizuri katika mchezo dhidi ya Jwaneng, alikuwa anahadaa sana mabeki pinzani na kujikuta viungo wa Simba wakipata nafasi," alisema Ambangile.

Mchezo huo uliwawezesha Simba kutinga hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuibuka na ushindi wa 6-0.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live