Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hii ndio sababu ya kocha Azam FC kunyimwa tuzo

Ongala Azam Bn.jpeg Kocha wa Azam FC, Kally Ongala

Thu, 8 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamati ya Tuzo za Shirikisho la Soka Tanzania TFF, imethibitisha kuwa haikuihusisha klabu ya Azam katika mchakato wa Kocha Bora wa mwezi Novemba, kutokana na kutokuwa na Kocha Mkuu katika mwezi huo.

Ufafanuzi huo unakuja baada ya Kamati ya Tuzo za Shirikisho la Soka Tanzania TFF kutangaza majina ya mchezaji bora wa mwezi Novemba ambayo imekwenda kwa Mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele na Kocha Bora akiwa ni Juma Mgunda kutoka Simba SC.

Kuna waliiona kuwa tuzo hiyo haikustahili kwenda kwa Mgunda kwa sababu Kally Ongala amefanya vizuri mwezi Novemba akiwa na Azam FC akicheza michezo mitano na kushinda michezo yote.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live