Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hii ndio sababu Waarabu kusajili Mastaa

Al Nssr Ronaldo.jpeg Hii ndio sababu Waarabu kusajili Mastaa

Tue, 26 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Saudi Arabia imeonekana kufuata nyayo za Nchi nyingine kadhaa kama vile China na Qatar katika kuwekeza kiasi kikubwa cha pesa na kujaribu kugeuza Taifa hilo kuwa visiwa kikubwa cha soka Ulimwenguni.

Katika dirisha la uhamisho lililovunja rekodi, vilabu vya Saudi Pro League (SPL) vilitumia takriban dola bilioni 1, kupata Mastaa bora zaidi ulimwenguni 94 kutoka ligi Kuu za Ulaya Ligue 1 ya Ufaransa, La Liga ya Hispania, Serie A ya Italia, Bundesliga ya Ujerumani na Ligi Kuu ya Uingereza hii ni kwa mujibu kwa kampuni ya Deloitte.

Kwa mujibu wa PIF, nia ya vilabu vya Saudia kuwasajili Mastaa wakubwa wa soka ulimwenguni ni pamoja na kuongeza ushindani ndani na nje ya uwanja, ambao Wachezaji wengi ambao wamesajiliwa kwenye vilabu vya Mfuko wa Taifa wa Uwekezaji wa Serikali (PIF) ili Mastaa hao wasaidie kukuza vipaji vichanga vya Saudia.

Wachezaji wote wapya walionunuliwa wanaungana na Mshindi wa tuzo ya Ballon d'Or mara tano, Cristiano Ronaldo, ambaye ana mkataba wa miaka miwili na Al-Nassr ambapo ataingiza kiasi cha dola milioni 200 kwa mwaka na kumfanya kuwa Staa anayelipwa zaidi Duniani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live